Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

Wadau wapinga Rais Samia na Makamu wake kuingia na Viti binafsi Kanisani, yadaiwa ni kujikweza

CHADEMA iliyotetemesha watawala ilikuwa ile ya enzi ya Dr Silaa. Iliwapa Watanzania matumaini ya kutokea kwa mabadiliko ya uhakika ya kisiasa. Hii ya sasa iko "diluted".
Dr Slaa tulimkaribisha sisi na kumlea
 
Uku Tu ndio Mambo haya yanatokea ......kule uingereza hawakuwa na shobo kabisa .........kamatia SITI ukae ukiona limejaa piga Chini utatembea aijalishi umbali
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere , iliyofanyika huko Mkoani Kagera , Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake , Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo .

Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe , lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi , huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee , Ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE , ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine .

Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla , na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena , kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa , basi wasiingie kwenye Makanisa , waishie nje na hotuba zao .

Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa , mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu , Hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa ?

View attachment 2387287

Angalizo : Sina chuki yoyote na viongozi hawa .
Mabenchi yasiyo na sponji yanaumiza.Au ungependa kuwaona waheshimiwa wamekunja sura kwa maumivu ya kukalia mbao mkuu?😂😂😂😂
 
Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa ,
Ziweke kama zipo hizo picha kibao za Joe Biden na Hichilema wa Zambia wakiwa kwenye mabenchi kanisani.... A picture is worth a thousand denials.
 

Attachments

  • IMG_20221014_232246.jpg
    IMG_20221014_232246.jpg
    33 KB · Views: 3
Mkuu mimi nakuunga mkono siku zote ila kwa hili sidhani kama inabidi liwe ishu sana, hajawahi kufanya hivyo kabla so inawezekana kuna harufu sio nzuri wat wa Usalama wamenusa, hiyo ni kazi yao, tuache wenye kazi yao waifanye, likitokea la kutokea ni sisi hao hao tutakaosema National Security ni wazembe, CCM ya leo sio ile ya Mwalimu Nyerere.
SASA hao watu wa usalama hawana iman na viongozi wa dini duuuh kwa lugha nyepesi kanisa haliaminiki hahahaha
 
Hii nchi watu wana obsession na mambo yasiyo na msingi.

Kiti gani Rais amekalia, inageuka topic.

Watu wanadhani Rais anaamka asubuhi na kusema leo nataka nikakalie kiti fulani! Never, hizo ni kazi za watu.
basi hao watu hawana kazi wapuuzi flani tu.,
 
Mfalme Henry VIII alikuwa mfalme wa kipekee aliyejua kucheza siasa ndani ya kanisa na ilipokuwa lazima kulichezesha kanisa ndani ya siasa. Kila alichofanya ilikuwa muhimu kiwe na sura ya kisiasa na kwa manufaa binafsi ya kisiasa. Alitumia bunge lake kuvunja kanuni ya kanisa ili aoe mke aliyezuiliwa na kanisa asimuoe. Moto ulipowaka sana aligeuka kuwa mwana matengenezo wa kanisa la Uingereza na kuachana na Papa. Alikuwa mfalme wa kipekee sana.

Hivi nilitaka kusema nini.....?! Ni hivi, Henry VIII ni mwanasiasa kweli. Wanasiasa aina ya mfalme huyu ni kama walinda mlango katika "eneo la kujidai". Eneo la kujidai ni eneo lile uwanjani karibu na goli ambapo mlinda mlango anaweza kubaki na mpira bila kubughudhiwa. Hata kama inakera kwake si kitu.

Wanasiasa mfano wa Mfalme Henry VIII wako hivyo. Hafanyi kitu chochote bila kukiingiza ktk eneo la kujidai kisiasa. Hata kama hamtaki na hata kama inakiuka taratibu si kitu. Kila kitu na kila mahali ni siasa tu.
 
Mada nyepesi sana. JPM alikalia kiti cha kwake alicholetewa na wasaidizi wake siku ile alipokwenda chuo kikuu na kuongea na wasomi hakuna aliyekuja na uzi kabisa.

JPM alikwenda chuo kikuu katika official capacity yake.

Kiongozi akienda kanisani anakwenda kama muumini, haendi kama kiongozi wa Serikali.
 
Back
Top Bottom