Kwenye Ibada Maalum ya kumbukumbu ya miaka 23 ya kifo cha Mwalimu Nyerere , iliyofanyika huko Mkoani Kagera , Viongozi kadhaa wa Kitaifa wamehudhuria, akiwemo Mh Rais Samia Suluhu na Makamu wake , Dr Philipo Mpango , Tunawapongeza kwa jambo hilo .
Sitaki kurudia yaliyotokea ili nisiwachoshe , lakini Kitendo cha Rais na Makamu wake kuingia na Viti vyao vya enzi ndani ya kanisa kimepingwa na wadau wengi , huku wakitahadharisha viongozi kuacha kujiona ni wa kipekee , Ukweli ni kwamba HAWANA UPEKEE WOWOTE , ukiachilia mbali vyeo walivyo navyo hawana tofauti yoyote nyingine na sisi wengine .
Kitendo cha kuingia na Masofa yao Kanisani ni DHARAU KWA WAUMINI na Kanisa kwa ujumla , na kinapaswa kukemewa ili kisirudiwe tena , kama hawataki kukaa kwenye mabenchi ya kanisa , basi wasiingie kwenye Makanisa , waishie nje na hotuba zao .
Ziko Picha kadhaa zikiwaonyesha Joe Biden wa Marekani na Haikainde Hichilema wa Zambia wakiwa wameheshimu madhabau na kukalia Mabenchi ya kanisa , mbona walishiriki ibada na wakamaliza kwa amani tu , Hawa viongozi wetu wana upekee gani hawa ?
View attachment 2387287
Angalizo : Sina chuki yoyote na viongozi hawa .