Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Wadau waulizia alipo Mwana CCM Thadei Ole Mushi

Noma sana ! Tumeonya wengi humu lakini hawatuelewi , Shetani hana rafiki
Kama ni kweli na mwathirika au watu waliyo karibu naye hawachukui hatua au kutoa tamko na wanaogopa mimi sioni umuhimu wa watu wengine kuingilia. Watanzania tumekuwa waoga kupitiliza na mtu hata ndugu yake akiuawa utasikia analalamika chini chini huku anasema ''msiseme lakini ni mimi nimelalamika''.
 
Kwahiyo unamanisha ccm wamempa sumu na wakamwita mkewe wakae wote sehemu ya Siri wauguzane

Thadeo na mkewe watoke waende muhimbili au penginepo
 
Kuna na yule mwingine alikua kayafa's chawa pro max anajiita Veronica France vip yupo na moto wake uleule kule jamuhuri ya Facebook?
 
Menbe alisema hatotekwa Wala kubufhudhuwa yeyote katika utawala huu wa Sa100.
 
Nimeona X-Mayor wa Ubungo Bwana Jacob akiripoti kwamba OLe MUSHI anaumwa na inasadikiwa amepewa sumu. Inaelezwa kuugua kwake ni siri na yupo Sehemu ya siri; wanadai wanasiasa wenzake wamemtenga na hakuna juhudi za kumfikisha hospital.

Nitoe rai kwa wanaohusika au familia watoke adharani kusema na jamii kuondoa uzushi huu unaolenga kubomoa taswira njema ya serikali ya kuwalinda wakosoaji wake. Serikali imejipambanua wazi kwamba haitishwi na wakosoaji hivyo ni vigumu wakosoaji wakapata madhara kiafya kisa wamesema vibaya chama au serikali.

Lakini pia nitoe wito kwa wanachama wa CCM kujiamini na kutosubiri maelekezo yakumsaidia binadamu anapopatwa na matatizo. Wenzenu CHadema wamewezaje kuwa wasemaji wema kwa wana CCM wanapougua au kupata majanga? Kwanini CHadema wawe wakwanza kutoa taarifa za msaada kwa mwana CCM?

Nape alipopata msaada marafiki wote wakamkimbia wakabaki wana harakati na CHadema kumsemea, same applies to mzee Kinana na hata akina polepole. Ninyi wahanga wanufaika wa siasa mnakosaje kujifunza kwa wenzenu?

Siasa zinapofika mahali zikakunyima uhuru wa kwenda msibani ,hospital au kwa mwanadamu mwenzako anayepitia kadhia flan basi hizo fikra za siasa zimekutenga na roho wa Mungu.

Kama ni kweli Ole MUSHI unaumwa tukutakie afya njema . Usisite kujitokeza kuomba msaada maana watu wema bado wapo na wanasubiri wito wako.
ok sawa
 
Back
Top Bottom