Naomba kujibu kwa faida ya wengi kipindi sisi tunabishana kuna watu wapo kimya wanaingiza pesa ya kutosha kwenye forex na wanaendesha maisha yao kupitia forex .Kwa uelewa wangu japo sio lazima ufuate kile ninachosema ,forex ni biashara kama biashara zingine tena ni biashara inayohitaji maarifa haswaa sio lelemama.tatizo unaweza kukuta mtu amesikia forex inalipa anajiingiza kwenye forex kichwakichwa bila kuwa na ujuzi wa kutosha kuhusu how to trade forex,matokeo yake anajikuta anashindwa na kupoteza mwishowe anaanza kulalamika na kuwaaminisha wengine kuwa forex ni kamali mara ni utapeli wakati mtu alishindwa kusoma na kupata maarifa ya kutosha ndio aingie sasa kwenye forex .Mwisho kwa dunia ya sasa kama unataka kufanikiwa kwenye jambo lolote tafadhali lifuatilie haswaaa soma,uliza,jaribu ndipo ufanikiwe.Narudia neno langu sio sheria unaweza ukafuata au ukaacha kufuata pia