King Kong III
JF-Expert Member
- Oct 15, 2010
- 56,205
- 79,515
Woow..hii safi sana,niyakumbukayo;
1. Ndala za "Skyway"
2.Raba za "DH"
3.Suruali za "Tokyo & Beauct"
4.Mafuta ya kujipaka "Rays"
5.Tanbond sio blue band
6.Soda ya double cola na fahari.
7.Negro arushaa aliitwa " Masawee"
8.Peugeot 403 & 404[emoji3]
Mama yangu mdogo alienda kusoma Ulaya akaja na TV, deki pamoja na mikanda ya akina Michael Jackson pamoja na Lionel Richie.
Daaah huyo jamaa noma. Bora angesema tu zimeunguaNishawahi fatilia picha almost mwezi mzima af nikaja ambiwa et zilivyosafishwa zilipeperuka
Nakumbuka ni juzi tu miaka ya 2007 Mara yangu ya kwanza kushonewa suti na shangazi ambayo hainitoshi ili nikue nayo nilipiga picha na dada yeye akiwa amechuchumaa nyingine tukapiga karibu na ua hivi vitu labda mtoto alie zaliwa mwaka 2009+ ndo anaweza kuwa hajakutana navyo[emoji16][emoji16]Enzi hizo upige picha ukishindwa kuikomboa basi jamaa ataibandika kwenye kuta za studio yake kama adhabu, hivyo tulihakikisha tunazikomboa kuepuka kuanikwa.
Nakumbuka pozi lilikuwa kuchuchumaa au kushika maua au kusimama miguu sawa kama upo paredi ya jeshi
Mkuu hili neno "Unju bin Unuq" ina maana moja na hilo jina lako/ID? Kwa maana ndio a.k.a ya rapper mmoja hapa bongo anaitwa Nikki Mbishi.Nishawahi fatilia picha almost mwezi mzima af nikaja ambiwa et zilivyosafishwa zilipeperuka
Mikoa mingine walikuwa wanaviita "saa sita utanikoma"...Viatu vya Cha Cha Cha unavijua?? Mwisho kuvivaa saa sita mchana.
Mwalimu J.K Nyerere alifariki mwaka 1999🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 mwaka huo nlikua mtu mzima, nakumbuka omar ali juma alifariki sjui alikuaga waziri a nn, nyerere anafariki mimi ndo nlikua nimetahiriwa
Ukiachana na haya ya album, hivi hawa watoto waliozaliwa juzi juzi wanajua kwamba hawa tunaowaita Wapiga debe jina lilitokana na kitu flani cha pembe nne kinachioitwa debe? Waliwahi kuliona debe? Siku hizi yapo wapi madebe wahenga?
Mkuu, bila shaka jamaa alikuwa anajaribu kusisitiza kwamba maisha ya enzi hizo hayakuwa digital sana kama sasa hivi.Sasa utamu na uharisia ni upi hapa hivi watanzania wanaweza sifia uzamani hata kama ulikuwa wakipuuzi au ndio niko serious sana.
Mimi ni wa mwaka 1984 kwa hiyo hawa wa mwaka 2003 nimewazidi miaka 19Dogo umeelewa vibaya. We utakuwa wa miaka 1998 kuzaliwa
Hahahahaaa na mkanda kujaa ni baada ya weeks kadhaa kupita...Hapo kwenye picha, utasikia hii siwezi kukupa kwa sababu nega yake haipo.
Na ilikuwa inachukiza kweli, umepiga picha leo unaipata baada ya mwezi, kila ukikutana na mpiga picha anakwambia mkanda haujajaa.
Wapangaji wenzangu ndio huwa wanatazama sio mimi mkuuKilichonishtua ni kujua kuwa unatazama tamthilia ya Sultani!
early 90's, enrique alianza kuimba miaka ya 90 mwanzon, hiyo sad eyes ni ngoma ya 94 , bailamos ni ya 99
Anaonekana bado ni kijana mdogo sanaAiseee...!!!! una umri gani?