Waendesha bodaboda, tabia hii inakera sana

Waendesha bodaboda, tabia hii inakera sana

Kwanini msitulie kijiweni mkawa mnabeba abiria wenu vizuri kwa zamu, akija abiria anaenda na huyu, akija mwingine anaenda na huyu mnakuwa na rotation nzuri kwa ustaarabu ili kila mtu apate mkate wa kila siku hizi papara zenu zina boa bana.
Wana viongozo wao wa Kitaifa na kimaeneo, wanatakiwa kutazama jambo hili ni kero kwa watu wengi, na mbaya zaidi huwa hawana utamaduni wa kumsalimu abiria kabla hawajamuuliza endapo anahitaji usafiri.

Jambo jingine linalokwaza ni uchafu, hawapigi mswaki wala kusafisha kwapa
 
Habari wakuu,

Niende moja kwa moja kwenye maada.

Hivi sasa tunatambua bodaboda imekuwa ni kazi inayowasaidia vijana wengi sana kujikwamua kiuchumi katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kitu ambacho ni kizuri sana.

Lakini kazi hii baadhi ya maeneo inafanywa kwa kukosa weledi na maarifa ya kibiashara, sijui ni kwa sababu wamekuwa wengi sana au tatizo nini?

Nakereka na tabia ya vijiwe vya bodaboda yaani mtu ukitokeza tu kwenye kona wanaza kukupigia honi na miluzi utafikiri mbuzi au mbwa kaiba mboga wengine kukukimbilia hovyo hovyo. Hivi kwanini msitulie tu kijiweni abiria si tunajua mnapopatikana.

Saa nyingine maeneo ya usafiri ukishuka tu kwenye gari kelele kibao za bodaboda na ukizubaa tu mara huyu kasha chukua na begi yaani tabu tupu.

Kwanini msitulie kijiweni mkawa mnabeba abiria wenu vizuri kwa zamu, akija abiria anaenda na huyu, akija mwingine anaenda na huyu mnakuwa na rotation nzuri kwa ustaarabu ili kila mtu apate mkate wa kila siku hizi papara zenu zina boa bana.

Nawapongeza bodaboda wa Mwanza na Tabora kidogo watulivu na hizi tabia ni chache kwao kama sio hawana kabisa.

Lakini baadhi yenu badilikeni, Pia vaeni vizuri hiyo ni kazi kama kazi nyingine mnajirundika makoti machafu na kofia za hovyo na hiyo miziki ya ajabu ajabu tena kwa sauti ya juu plus kuendesho hovyo.
Waafrika wote sisi tunashida hapo kwenye kuweka mtiririko wao kupokea abiria kwa utaratibu mmmmh ni shida. Ukifika stendi tu sisi wenyewe tunavyoingia dirishani, kupigana vikumbo mlangoni utajua tu hatuko sawa.
 
Nachukizwa sana pale bodaboda anapopakia abiria halafu mziki sauti mpaka mwisho...wanafikiri abiria wote wapenda heka heka.

Hii tabia ya kudaka daka watu hovyo imeibuka pia pale Makumbusho (Dsm)stand...ile migahawa pale around.
Kuondoa hiyo kero ya kudakwa dakwa,tumia bodaboda wa bolt au uber kwanza gharama ni nafuu halafu wanajua wafanyacho.
 
Umeongea kila kitu mkuu hawa watu hawajielewi azura zimewatawala.
 
Mmesema mengi ila kuna sisi boda wastaarabu. Ila kweli wenzetu wengi wanatuharibia sifa ya hii kazi yetu.
 
Wengine hata boksa na chupi zao zinanuka halikadhalika midomo na meno ndio usiseme ni shiidaaa kubwa.
Na wengine kutwa nzima anatembea na toothpick mdomoni.
Wengi wa bodaboda ni washamba sana.!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan watu wanatema cheche hatareeeh. Lol
 
Mimi nikishuka kwenye daladala hawa hapa, wanasahau natembea tu kuingia kazini kwangu....au nikiwa na gari yangu nikishuka kwenda kununua vocha hawa hapa, tayari wameshasahau nimeshuka kwenye ndinga yangu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wengine hata boksa na chupi zao zinanuka halikadhalika midomo na meno ndio usiseme ni shiidaaa kubwa.
Na wengine kutwa nzima anatembea na toothpick mdomoni.
Wengi wa bodaboda ni washamba sana.!
Ni kweli kabisa Mkuu sisi ni washamba ila wake na madem zenu wanapenda sana kuleta shobo ili tuwagonge nao, sijui kwanini?!
 
Back
Top Bottom