Wafaham Vijana wa kampeni ya "Kataa Ndoa " !!

Binafsi nikishaona mtu anasema OA sababu eti ukiwa mzee utatunzwa na mkeo, namuona ni mjinga sana. Anasahau hatujui tutakufa lini na nani atatangulia.

Unaweza ukaoa, ukawa na watoto na bado wote wakakuacha hapa duniani unateseka na upweke.

OA ukitaka KUOA, na sisi HATUOI sababu HATUJATAKA KUOA. Tukitaka TUTAOA pia bila kelele
 
You have some point lakini umejichanganya sana.

Kwanza kabisa kuowa au kuolewa siyo lazima, Mimi ni mwanandoa na Nina Watoto kwahiyo soma kwa makini ninachokiandika.

Ukiowa kweli mke uliyepewa na Mungu hesabu umetobowa maisha hata uwe huna kitu lazima mtobowe nimeona mengi, tena Nina maslahi na hili first born wangu ni mtoto wa kiume na tayari yupo Chuo sintofurahi aingie mkenge wa kuowa kufurahisha watu.

Pili ukisema vijana wanapenda kazi laini laini unakosea, tumetumia gharama kubwa sana kuwasomesha private school ni mategemeo yangu watumie akili zaidi kutengeneza maisha yao, kama maguvu yanalipa basi wabeba zege wangekuwa ndio watu waliofanikiwa zaidi wakifuatiwa na wabeba Lumbesa.

Kwenye mambo ya kiimani hili lawama tunabeba Wazazi moja kwa moja ndio wenye wajibu kama tumefeli usitegemee vijana hawa miaka ya 2000 kama wana maajabu yoyote, wengi wamezaliwa na roho tu lakini nafsi hawana, itakuchukuwa muda sana kuja kuthibitisha hili kwamba kizazi hiki vijana wengi hawana nafsi wana roho tu, hilo ni tatizo kubwa sana.

Ningeandika mengi lakini naona nitakuchanganya tu, in short wanahitaji msaada zaidi kuliko kuwasema.
 
Kinachoshangaza zaidi ni pale ambapo wanaoumizwa na kampeni ya KATAA NDOA ni wale walio kwenye NDOA. Asili ya muafrika akiwa anapitia kwenye wakati mgumu huwa anatamani kila mtu apitie magumu wawe wengi. Kila mtu aishi kwa namna anavyoona inamfaa, tusipangiane maisha.
 
Mwanaume kukimbilia ndoa ni kukimbilia kifo tena cha mateso. KATAA NDOA
NDOA NI UFIRIMASO
KATAA NDOA
NDOA NI USHETANI
KATAA NDOA
NDOA NI DECI/KILIMO CHA VANILLA/QNET

Leo nimeamua kujiunga rasmi na hii movement, nipokeeni
Umenichekesha kinoma eti Ufirimaso 😂🤣 Ila enewei Karbu kwny Kampeni yetu
 

Kama kweli hizo ndo sifa zao, unafanya kosa kubwa sana kuwashauri waoe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…