Jimbo la Muheza, Chadema na ACT mkiunganisha nguvu mnachukua asubuhi kabisa...kunakwenda kutokea kura za hasira..
Shinyanga mjini, Chadema na ACT mkiunganisha nguvu mnashinda asubuhi tu, Katambi Chadema ilimbeba kipindi kile hana nguvu Shy pale.. Madon wa Shy bila shaka watasimamia show hasa kwa kukatwa vijana wao Masele na Gasper..
Kawe, with fair and free election kazi ni rahisi sana kwa Halima, Jimbo la kawe tayari CCM wamegawanyika lakini pia hakuna mwenye akili timamu pale kawe anaweza kuchagua opportunistic Gwaji boy.
Mbeya, with fair and free election, Sugu anashinda..Tulia hakubariki kiasi cha kupata kura za kumzidi Sugu.. Mbeya wapiga kura ni vijana na wazee wa kati ambao wengi wao ni wahangaikaji wasioipenda CCM na sera zake kifuli hawaitaki tu CCM.
Arusha, with fair and free election, Lema anashinda pamoja na Gambo kutumia rasimali za serikali na mbeleko kufanya kampeni miaka mitano bado ni kazi ngumu kumnadi Arusha na kupata kura zaidi ya Lema.
USHAURI: WAPINZANI FUNGUENI KESI KUWAWEKEA PINGAMIZI TULIA NA GAMBO KWA KUFANYA KAMPENI KWA MIAKA MITANO KWENYE MAJIMBO AMBAYO WANAGOMBEA SASA, PIA WAMETUMIA RASILIMARI ZA NCHI KUPIGA KAMPENI KWA MIAKA MITANO.. WEKENI PINGAMIZI MAPEMA USHAHIDI UKO WAZI..