Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Huyu ndiye mbunge wa CCM aliyetoa hotuba kali kuonyesha kukerwa kwa tukio la kushambuliwa Lissu. Akateuliwa kuongoza tume maalum ya bunge kuchunguza tukio lile japo matokeo yakazuiwa kutangazwa kutoka huko juu.

Huyu japo alishinda kura za wajumbe ila amekatwa na mwana fa kubeba mzigo.

Kuna kitu nyuma ya pazia.

Naamini sasa ukweli utawekwa peupeee na kivumbi kitatimka kweli kweli.
Naona Mods wameunganisha uzi kukwepa nyundo.
 
Jimbo la Muheza, Chadema na ACT mkiunganisha nguvu mnachukua asubuhi kabisa...kunakwenda kutokea kura za hasira..

Shinyanga mjini, Chadema na ACT mkiunganisha nguvu mnashinda asubuhi tu, Katambi Chadema ilimbeba kipindi kile hana nguvu Shy pale.. Madon wa Shy bila shaka watasimamia show hasa kwa kukatwa vijana wao Masele na Gasper..

Kawe, with fair and free election kazi ni rahisi sana kwa Halima, Jimbo la kawe tayari CCM wamegawanyika lakini pia hakuna mwenye akili timamu pale kawe anaweza kuchagua opportunistic Gwaji boy.

Mbeya, with fair and free election, Sugu anashinda..Tulia hakubariki kiasi cha kupata kura za kumzidi Sugu.. Mbeya wapiga kura ni vijana na wazee wa kati ambao wengi wao ni wahangaikaji wasioipenda CCM na sera zake kifuli hawaitaki tu CCM.

Arusha, with fair and free election, Lema anashinda pamoja na Gambo kutumia rasimali za serikali na mbeleko kufanya kampeni miaka mitano bado ni kazi ngumu kumnadi Arusha na kupata kura zaidi ya Lema.

USHAURI: WAPINZANI FUNGUENI KESI KUWAWEKEA PINGAMIZI TULIA NA GAMBO KWA KUFANYA KAMPENI KWA MIAKA MITANO KWENYE MAJIMBO AMBAYO WANAGOMBEA SASA, PIA WAMETUMIA RASILIMARI ZA NCHI KUPIGA KAMPENI KWA MIAKA MITANO.. WEKENI PINGAMIZI MAPEMA USHAHIDI UKO WAZI..
 
Bavicha mnachezeshwa ngoma ya ccm. Mwaka huu mavi yatapita kooni, mark my words
 
Ni haki yake na anafaa upinzani sababu ni critic ila hasira za hivi hazina mwisho mzuri. Siasa zina hesabu zake, hata akienda upande mwingine kwa CCM ya awamu hii atashindwa tu! Akijichanganya tu ameharibu mazima.
Hakuna ccm mdebwedo kama hii , mambo ya kuua na kuteka hayana nafasi tena , kwa sasa ni hoja tu
 
Upinzani fungueni kesi kuishitaki CCM kwa kufanya kampeni kwa miaka mitano kwa kutumia rasirimali za Watanzania kwa manufaa ya CCM. Kipindi chote cha miaka mitano CCM wamefanya kampeni huku vyama vingine vikizuiwa.

Lakini pia kuna baadhi ya majimbo wagombea wateule wa CCM walishaanza kufanya kampeni tena kwa kutumia nyadhifa zao na rasimali za watanzania wakisaidiwa pia na viongozi wa Serikali.
 
Wewe unasema mwana FA , Patrobas Katambi alikuwa wa mwisho kura 12 lakini ndio kapitishwa unacheza na chama Cha makanikia ya kijani.
Screenshot_20200820-185954.png
 
Takribani kwa baadhi ya mikoa wamechomekea aliyeshindwa mmoja . Hii ina maana kubwa sana. Wapo makini sana kwa sababu hapo wanachanga karata zao kwa kutesti mitambo. Ni dhahiri hayo majimbo wameyaweka rehani endapo uchaguzi utakuwa wa haki .

Wamejaribu kuwapa imani waunga juhudi kwamba wamethaminiwa japo kutoboa bila mbeleko ni kazi kubwa sana kwao.

Wanajua kutakuwa na mtifuano kati ya waliopita kura za maoni na wateule hivyo wamefanya uamuzi huo kwa makusudi kwa baadhi ya mikoa ili wasiathirike sana.
 
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo,

Adadi Mohammed Rajabu Meta, mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa zamani, mbunge wa jimbo la Muheza aliyemaliza muda wake, pia aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya ndani na usalama...
Km ni kweli hiyo ndiyo sababu ya kunyimwa uteuzi basi Mungu atafanya kazi yake . Daima ukweli hudumu na kamwe hauchanganyiki na uongo.

Daima haki hushinda uovu.
 
Wakuu nawasalimu,

Mwanamama Faith Mitambo wa jimbo la Liwale Lindi aliongoza kura za maoni kwa kuwagaragaza wanaume lakini cha kushangaza mama huyu amekatwa na kupewa mshindi wa pili wakati tunapambana kuhakikisha wanawake tunawapa kipaumbele binafs hii naiona kama dosari kubwa sana
 
Tuseme ukabila umembeba askofu Gwajima,?nauliza kwasababu hakuwa mshindi wa pili,walio mzidi kwa kura wameondolewa kwa kigezo gani?ukisema rushwa nitakukatalia kwa kuwa wapo walio kamatwa live na waliotoa rushwa waziwazi majina yao yamerudi,Sasa kwa Nini Kawe au ndio usukuma?
Niamini mimi mkuu kama kuna watu waliotoa rushwa Kawe basi Askofu katoa hela nyingi kuliko wagombea wote nilikuwa karibu sana kwenye huu mchakato
 
Wanaoshinda hapo ni Kimei na mwana FA tu. Gwajima na Silinde hawashindi ata iweje na sababu ni kuwa wanagombea majimbo magumu sana yenye watu wagumu sana!!
Unakumbuka kilichompa Lwenje na Kafulila? Weka hakiba ya maneno.
 
Back
Top Bottom