Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Masele hana jeuri hiyo tatizo lake anayo makando kando mengi ya huko nyuma alipo kuwa Naibu Waziri wa madini
Hili jambo ndilo hata me lianifanya niamini hawezi hama, kimsingi kamezeshwa ndoano na atatakiwa kumnadi Katambi ambaye alimshinda kwa hila 2015.
 
Tunahitaji viongozi safii wasio na doa kama kapumzishwa Chenge na Adadi yeye ni nani asisubiri!
 
Ni haki yake na anafaa upinzani sababu ni critic ila hasira za hivi hazina mwisho mzuri. Siasa zina hesabu zake, hata akienda upande mwingine kwa CCM ya awamu hii atashindwa tu! Akijichanganya tu ameharibu mazima.
Pia yeye mwenyewe alivyopata Hilo Jimbo Kwa eti Kura moja haikuwa very convincing..akihama atafanyiwa figisu kama zilizompatia yeye ushindi 2010.
 
Hata kama ni mimi yaani nishinde , halafu wa mwisho ndio anateuliwa chama kijani kibichi hamnazo kabisa
Screenshot_20200820-185954.png
 
Ni haki yake na anafaa upinzani sababu ni critic ila hasira za hivi hazina mwisho mzuri. Siasa zina hesabu zake, hata akienda upande mwingine kwa CCM ya awamu hii atashindwa tu! Akijichanganya tu ameharibu mazima.
CCM ya awamu hii inayominya uhuru wa raia kama North Korea
 
Huyu ndiye mbunge wa CCM aliyetoa hotuba kali kuonyesha kukerwa kwa tukio la kushambuliwa Lissu. Akateuliwa kuongoza tume maalum ya bunge kuchunguza tukio lile japo matokeo yakazuiwa kutangazwa kutoka huko juu.

Huyu japo alishinda kura za wajumbe ila amekatwa na mwana fa kubeba mzigo.

Kuna kitu nyuma ya pazia.

Naamini sasa ukweli utawekwa peupeee na kivumbi kitatimka kweli kweli.
 
Anaandika Dr. Christopher Cyrilo,

Adadi Mohammed Rajabu Meta, mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa zamani, mbunge wa jimbo la Muheza aliyemaliza muda wake, pia aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya ndani na usalama.

Huyu aliwahi kuitaka serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani itoe maelezo ya kutosha kuhusiana na matukio ya utekaji, utesaji na mashambulizi kwa viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge. Ni baada ya tukio la kushambuliwa Tundu Antipass Lissu.

Akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya ndani, ulinzi na usalama, ripoti yake ya uchunguzi wa matukio ya utekaji na mashambulizi yaliyofanywa na watu "wasiojulikana" ilinyofolewa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hukohuko bungeni.

Kwenye kura za maoni alipata kura 597, dhidi ya mtia nia mwingine Hamis Mwinjuma (Mwana FA) aliyepata kura 296.

Hamis Mwinjuma ameteuliwa kuwania ubunge Jimbo la Muheza.

Nampongeza Hamis Mwinjuma kwa kupewa nafasi hii ya kugombea ubunge nyumbani kwetu Muheza. Lakini niseme tu kwamba mazingira ya kupata nafasi hii si mazuri sana. Kijana kama anayajua mambo haya basi atakuwa mtu mwenye kutafakari sana wakati huu, ila kama haelewi atakuwa mwenye furaha. Kuhusu ushindi, kwake litakuwa jambo la bahati.

Tukutane Muheza!
View attachment 1543273View attachment 1543274
It is a pity! Blood bastard hopeless CCM
 
Back
Top Bottom