Anaandika Dr. Christopher Cyrilo,
Adadi Mohammed Rajabu Meta, mkurugenzi mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai wa zamani, mbunge wa jimbo la Muheza aliyemaliza muda wake, pia aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya mambo ya ndani na usalama.
Huyu aliwahi kuitaka serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani itoe maelezo ya kutosha kuhusiana na matukio ya utekaji, utesaji na mashambulizi kwa viongozi wa kisiasa wakiwemo wabunge. Ni baada ya tukio la kushambuliwa Tundu Antipass Lissu.
Akiwa kama Mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia mambo ya ndani, ulinzi na usalama, ripoti yake ya uchunguzi wa matukio ya utekaji na mashambulizi yaliyofanywa na watu "wasiojulikana" ilinyofolewa na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, hukohuko bungeni.
Kwenye kura za maoni alipata kura 597, dhidi ya mtia nia mwingine Hamis Mwinjuma (Mwana FA) aliyepata kura 296.
Hamis Mwinjuma ameteuliwa kuwania ubunge Jimbo la Muheza.
Nampongeza Hamis Mwinjuma kwa kupewa nafasi hii ya kugombea ubunge nyumbani kwetu Muheza. Lakini niseme tu kwamba mazingira ya kupata nafasi hii si mazuri sana. Kijana kama anayajua mambo haya basi atakuwa mtu mwenye kutafakari sana wakati huu, ila kama haelewi atakuwa mwenye furaha. Kuhusu ushindi, kwake litakuwa jambo la bahati.
Tukutane Muheza!
View attachment 1543273View attachment 1543274