Kuna dhana imejengeka kwamba kila anayevaa vazi la kanzu ni muislamu au mwarabu, kumbe si kweli, unaweza kumkuta mtu amevaa kanzu kumbe wala si muislamu kabisa. Miaka ya nyuma nilikuwa na safari nyingi za kikazi Unguja, na kila wikiendi wakati wa jioni hasa Ijumaa na Jumammosi nilipendelea kwenda Bwawani Hotel, wakati huo ndio kilikuwa kiwanja maarufu kwa ajili ya muziki wa disco, vyakula na vinywaji 'aina zote' na 'watu aina zote'. Wikiendi moja usiku mwingi nilikuwa nimekaa na wenzangu hapo Bwawani tukipata 'vyombo', na meza ya jirani walikuwepo 'waarabu watatu' wakiwa wamevaa kanzu huku wakiwa wamezungukwa na 'machangu kibao' na mezani kwao kukiwa kumefurika pombe za kila aina. Ni Taswira ambayo ilituchanganya wengi usiku ule. 'Waarabu' wale wanawezaje kunywa pombe na kuzungukwa na makahaba kwa uwazi bila kificho, tena kisiwani Unguja!!?? Ilitushangaza wengi, hata baadhi ya 'wenyeji' walianza kuhisi 'wanakwazwa' na uwepo wa 'waarabu' wale na vituko vyao. Ilibidi 'mwenyeji' mmoja aende kumwita polisi kuwahoji 'waarabu' wale kisa cha kuonesha tabia ile. Ilichukuwa dakika 2 tu 'kuimaliza kesi ile. 'Waarabu' wale walipoulizwa wakasema, wao si waarabu na wala si waislamu bali ni wakristo na wanatokea Lebanon, na aina ile ya mavazi kwao ni mavazi ya kawaida kabisa. Na wako Unguja kikazi, wanafanyakazi melini na kwa wakati huo meli yao ilikuwa ikishusha mizigo bandarini, nao wakaamua kuja Bwawani kujirusha.
Tangu siku ile nimejifunza kwamba si kila anayevaa kanzu ni mwarabu au muislamu.
Tangu siku ile nimejifunza kwamba si kila anayevaa kanzu ni mwarabu au muislamu.