Wafahamu waarabu/usiyoyajua kuhusu waarabu

Wafahamu waarabu/usiyoyajua kuhusu waarabu

Naona watu wanahangaika sana, kwanza niwe muwazi, binafsi mimi ni muislamu, naweza kuchangia hiki kidogo nilichonacho

Uislamu ni kitu kingine na mwarabu ni kitu kingine, mwarabu nae ni binadamu km alivyo hussein wa nyamisati, andrew wa kwa mtogole na chausiku wa k/koo, so hakuna mkamilifu, mkamilifu ni mungu pekee yake, nakiri kuna waarabu safi na waarabu washenzi tena wale washenzi waliopindukia na hii ni moja ya sababu mitume mingi kupelekwa kule sababu ya ushenzi wao, binafsi naamin mitume ilipekwa pale kwa sababu kuu 2, japo kuna visababu vinhine vidogo vidogo kadhaa ila hizi mbili naona ni za msingi
1. Sababu ya ulimwengu kuanzia hapo, yaani kazi ya mitume ilikuwa ni kufundisha ya mungu, kukataza mabaya na kufundisha mema ili tupate kuishi vyema, kwahiyo manabii km nuhu na wengi wa mwanzo naamini walipelekwa pale sababu ya uwepo wa watu maeneo yale sitaki kuamin kipindi cha nuhu eti watu walikuwa wamesambaa mpaka china, amerika ya kusini huko au australia hapana, watu walikuwepo pale na ndio maana lina nuhu wakawepo pale

2. Sababu ya pili hii ni kutokana na ushenzi wa waarabu, sababu mitume mingi km kina muhammad na wengineo waliletwa kipindi ambacho dunia imesambaa,hata koguryeo ilikiwa tayaar imeexist, sehemu mbali mbali watu walikuwa tayar wameanxisha makazi mpaka africa watu tayar walikuwepo, sasa tujiulize waarabu walikuwa safi au washenzi mdio maana wakapelekewa mtume, mbona hakupelekwa hata kwa kina jumong, inawezekana mungu aliona hawa wengine wana moyo laini watapokea mafunzo, ila pia kikiharibika kizazi pale ulimwengu na mitume mingi imepitia basi ulimwemgu utaharibika kwa kiasi kikubwa(mungu ndio amajua zaidi) kipindi muhammad anakuja kuikamilisha kazi waliofanya kina nuhu, salehe, zakaria, daudi,yusuf, yakubu, yahaya, ayubu ibrahim, suleimani, mussa, issa bin marym na wengineo, ukichunguza hawa mitume wengi walikutana na visa, mikasa na ujeuri mkubwa wa watu wa mashariki ya kati, enzi za ujahilia kabla mtume kuna watu walikuwa wanazika watoto wa kike, kuna watu walikuwa wanabet kabisa kuwa mimba ile ni mtoto wa kiume ama wa kike nakupelekea kujikuta wanampasua huyo mwanamke ili kupata kuhakiki kilichomo, hebu we fikiria mwenyewe, na mambo kibao ambayo mtume muhammad(s.a.w) alikuja kuyakataza na kuleta sheria km nilivyosema alikuja kukamilisha kazi za mitume minginie na ndio maana karibia na kifo chake alisema ametukamilishia dini yetu, yaani alikuja kuweka viraka na kuziba mule kwenye mapungufu mfano katika torati ya musa kuna vitu vichache mnoo yeye alikuja kuongezea nyama mule kulipo pungua na kuleta ya ziada na kiada(nimekumbuka shule ya msingi) katika zaburi ya daudi na injili ya issa bin mariam pia kuna vitu havikuwemo yeye alikuja kuviweka sawa kukamilisha dini maana baada ya yeye hakukuwa na mwingine wa kuja ndio maana katika quraan unakutana na maelezo mengi, quraan imeelezea na kutufunza vingi baadhi ya vitu vichache ambavyo quraan ima imetolea maelezo au imetufunza ni

Ndoa(17)
Haki(16)
Madaraka/mamlaka(3)
Watoto(22)
Mavazi(7)
Wanyama(8)
Ndugu(25)
Wake(22)
Wanawake(41)
Interest(7)
Wealth(37)
Yatima(19)
Ujirani(1)
Ndoa(17)
Utu(28)
Tabia(9)
Kifo(11)
Maradhi(12)
Zawadi(24)
Kusamehe(28)
Vinywaji(11)
Talaka(5)
Rushwa(10)
Crime(65)
Earthquake(11)
Hivi vyote tumefunzwa vimeelekezwa ndani ya quraan na vingine vingi vingi.

Quraan pia imezungumzia mambo ya kisayansi mie napenda kuita science facts, quraan imezungumzia
1. Sky as a protector
2.function of mountains
3. Movements of mountains
4.orbits
5.wormholes
6. Atoms
7. Expanaion of universe
8. Sex of baby
9. Cerbrum
10.time relativity
11. Presence of iron
12deep sea and internal waves
13. Proportion of rain
14.identity of fingerprints
15 lowest point on earth
16. Pulsar and black hole
17. Clouds..

Hebu fikiria mtume alikuwa jangwani huko hakuwa mvuvi wala hakuwahi kufanya kazi za bahari ila kazungumzia bahari 2 zilizokitana bila maji yake kuchanganyana, mambo ya deep sea na internal waves, alizungumzia mambo yajayo km victory of romans, tujitahidi kusoma tujue ukweli wa mambo ile dhana ya ukitaka kumficha mtu ukweli uweke kwenye kitabu hapa huwa naiona saana.

Dhumuni halikuwa kuleta mambo ya udini katika uzi huu wa ndugu yangu, lengo lilikuwa ni kitofautisha baina ya uislam na mwaarabu, maana waislam wenzangu wanataka kufanya muarabu ndio awe nembo ya uislam kitu ambacho si kweli, enzi za nabii lut sodoma na gomora ilikuwaje si watu hao hao wa mashariki ya kati.. Waarabu nao ni watu km wengine kuna wema na washenzi pia. Niwatakie siku njema
Mkuu upo vizuri..much respect to you
 
Sultan said mwaka 1840


Ila walianza kitambo kabla ya hapa. Historia inasema waarab walianza kuua na kutesa waafrika wa Zanzibar toka karne ya 5 (500AD). Waliwachuku utumwani na kuwahasi wanaume ili wasizaane na kubaka wanawake as sex slaves. Wanaume wengi walitoswa majini baada ya kucoka kazi kutokana na uzee ama magonjwa maana walikuwa hawafai tena kwa mabosi wao.
 
Habari zenu watu wa JF..

Leo tupate kujua kidogo kuhusiana na hawa watu tunaowaita "Waarabu"...Nimepitia pitia kidogo nchi zao na pia kusoma vitabu vyao vinavyoelezea maisha yao...haya yafuatayo ndio niliopata kuyafahamu kutoka kwa "waarabu":-

1.Neno "uarabu"-"arab" ni neno linalowakilisha asili/tamaduni/culture na sio rangi kama wengi tujuavyo.

2.Duniani kuna nchi 22 za kiarabu,yani waishipo waarabu nazo ni-Lebanon,Syria,Morocco,misri,Tunisia,Iran,iraq,Jordan,kuwait,Qatar,Saudi arabia,Somalia,Djibouti,Comoro,Sudan,Palestina,Mauritania,Algeria,Oman,UAE,Bahrain na Yemen.

3.Waarabu wote sio Waislamu,Na Waislamu wote sio waarabu..ingawa kundi kubwa la waarabu ni waislamu,wachache sana ndio wakristo na Wayahudi.

4.Waarabu ni watu ambao wanawaheshimu sana Wazee na Watawala wao...Ni mwiko sana kukosoa,kudhihaki na hata kumfokea mtu aliyekuzidi umri au aliye mtawala wako.Wana Heshima yenye hofu kubwa yaweza ikawa kuliko taifa zingine zote.

5.Sio Mataifa yote ya kiarabu vazi lao la utamaduni ni kanzu,la hasha,bali yapo mataifa ya kiarabu ni nadra sana kumuona mtu kavaa kanzu nayo ni mojawapo Syria,Misri na Lebanon.

6.Kwenye Lugha ya kiarabu,lugha/ishara ya mwili(body language) ni kitu muhimu sana kuliko hata maongezi yenyewe..Pata muda tizama clips zao.

7.Lugha ya kiarabu ni miongoni mwa lugha inayozungumzwa kwa mfanano karibia mataifa yote ya kiarabu...mfano kwenye kiingereza kuna kiingereza cha wales,australia,marekani n.k

8.Sifa kubwa ya waarabu katika ulaji chakula ni "kutumia mkono" yaani no kijiko no uma..hata awe tajiri kiasi gani dhana yake ya kwanza kwenye kula ni "mkono wake"..Hii imepelekea kupenda kuwa na hotel/migahawa yao mahsusi.

9.Ukiwa kwenye mkutano/meeting ni mwiko kutizama saa iwe ukutani au mkononi,ukifanya hivyo ni ishara ya kuwadharau walioko kwenye mkutano.

10.Mahusiano ya kifamilia/undugu yana nguvu sana kwa waarabu..kwa mfano unaeza kuta nyumba moja wanaishi karibia ukoo/yani bibi wa bibi mpaka babu wa babu na wajukuu wake.

11.Umri hauna nafasi katika kujitegemea yani kuwa huru na makatazo au amri au huduma za wazazi..yani mtu anaweza akafika hata miaka 40 lakini akawa anahudumiwa na wazazi wake.

12.kwa kawaida uchukua zaidi ya mwaka na miezi saba kujua lugha ya kiarabu kwa ufasaha.

13.kinywaji kikubwa katika nchi za waarabu ni kahawa...

AHSANTENI NI HAYO TU YA KWANGU....MENGINE KUHUSU WAARABU NAHISI TUTAYAPATA KUTOKA KWA WACHANGIAJI...[emoji120]
Mzee kwa waarabu hii tabia ya kuoa mke zaidi ya mmoj ipo? Au waafrica tu ndo hukazania iko kipengele?
 
Kuna nchi nyingi za kiarabu umeziruka hapo MF.Libya na Sudan
 
Nataka kujua zaidi kuhusu wanawake wa kiarabu na taabia zao
 
Mkuu hujasoma shule au hata kujuwa history ya waafrika na Afrika as a whole? Somalians are Africans na si waarab hata wao wenyewe watakuambia hivyo.
basi nahisi utakuwa upo sekondari....tena form two...kwani morocco,algeria,tunisia na misri sio waafrika?..kama hujafika hata degree tuliza mpira
 
Sultan said mwaka 1840
Maskini ulivokosea, kama hamuijui Historia ya watu ni kheri kukaa kimya tu, ya huko kwenu wenyewe hamuijui akisha mnajifanya wajuaji ya wasiokuhusu.

haya nakufundisha historia kuwa, Mtawala wa Mwanzo Zanzibar ni Mreno... (Portugal). Naomba uende ukamsute mwalimu wako wa historia.
 
Umechangia Hoja Vizuri ila umeshangaza tu pale ulipoitaja chama chako CCM tu hivi huwezi changia hoja bila kutaja CCM.........??????!!!!!!
Mkuu CCM ya Zanzibar, inahusika moja kwa moja na kuichafua historia ya Zanzibar ili kulinda maslahi yao. Ndio maana nkaitaja CCM ya ZANZIBAR sio ya BARA. CCM ya Zanzibar siku za kampeni walikuwa wakimtukana Maalim Seif, wakidai kuwa anataka kurudisha Usultani. Ni wao ndio waliopindua Utawala wa barghash, ni wao ndio wanaohalalisha kitendo icho kupitia historia yao. Ni wajibu wao kuwaaminisha watu kuwa mapinduzi yalikuwa lazima yafanyike.

Ukiongea Historia ya Zanzibar akisha ukawa hujazungumzia vyama vya siasa, utakuwa umetoa mukhtasari tu lakini habari kamili hujaitoa.
 
Tatizo watu mnapenda kukosoa bila kuweka hadharani vyanzo vya taarifa zenu. Mna base zaidi kwenye oral tradition. Jambo ambalo ni risk kwa walaji wa taarifa.
Tuna wazee wetu ambao walikuwepo wakati huo Karume yupo Hai. Hata written tradition can be distorted. Historia ya Zanzibar iko very controversial.
 
Mkuu una hoja nzito za kuwatoa tongo Watanganyika wanaojiita maprofesa.
Mkuu, ukitaka wawe mabubu waambie wakuletee picha za mwarabu akiwa na mtumwa, utakuta za kuchora tu. Hata picha za watu wapo kwenye mashamba ya karafuu humkuti warabu akiwa na bakora.
 
Wazungu kufanya biashara ya utumwa haifuti fact kwamba waarabu walifanya ushetani wote ni kapu moja
Babu Yako alomuuza kakake hakuwa Shetani nae? Si alipewa kioo tu ajitizame akaona ana pacha mwenzake sasa akawa hana shida ya kakake akamuuza kwa wazungu? Nani shetani zaidi sasa hapo?
 
Babu Yako alomuuza kakake hakuwa Shetani nae? Si alipewa kioo tu ajitizame akaona ana pacha mwenzake sasa akawa hana shida ya kakake akamuuza kwa wazungu? Nani shetani zaidi sasa hapo?
Hakuna kitu Kama hicho waarabu walitumia mtutu,kuchukua watumwa na wewe kwa akili yako ya kushikiwa unaamini hizo habari za vioo,ukishikiwa akili yako umeshikiwa maisha yako

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna kitu Kama hicho waarabu walitumia mtutu,kuchukua watumwa na wewe kwa akili yako ya kushikiwa unaamini hizo habari za vioo,ukishikiwa akili yako umeshikiwa maisha yako

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
Lete ushahidi waarabu waliwashikia mtutu 😀 😀 😀

Nitajie nchi zilizotawaliwa na waarabu Afrika na zile zilizotawaliwa na wazungu Afrika
 
Back
Top Bottom