DOKEZO Wafanyabiashara Kariakoo kugoma Mei 15, 2023

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mkuu heshima kwako.

Unadhan nin kifanyike?, Kumbuka serikali haina uwezo wa kufanya biashara wala kuendesha viwanda.
Swali zuri sana.
Hili suala inatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu na uongozi bora. Pia upatikanaji wa mitaji kiurahisi ili kuanzisha viwanda mfano china wana mabenki maalumu kwa kila sector, Kuna benki ya viwanda, benki ya kilimo, benki ya wakandarasi e.t.c. Pia kuweka mifumo ya kulinda viwanda vya ndani.

Nahisi kuna uzi humu alielezea kwa kina mtaalam wa uchumi Naanto Mushi alielezea
 
Tanzania siku hizi limekuwa Taifa la Wachuuzi tu na si wazalishaji, kila Mtu siku hizi ni mfanyabiashara,tena biashara nyingi ziko kwenye mitandao hata fremu hakuna!!
 
Yupo Mkongo mmoja alikua anakuja kununua mzigo Kariakoo kakamatwa mara mbili akipeleka mzigo wake kwenye Fusso za Tunduma na risiti anapewa wanataka rushwa wanafungua mzigo wote ili wapate rushwa kahamia kununua SA anashangaa uhuru uliokuwepo nunua hata makontena mia wewe yape ulinzi tuu na si mambo ya kukwamishana kama Kariakoo...TRA wala rushwa ndio wanarudisha nyuma maendeleo ya Nchi kwa ubinafsi wao na wana kiwango maalumu cha rushwa...
 
Hili la usajili wa stoo hili ndio sababu ya huo mgomo wasisingizie urasimu bandarini
 
Bro hujui kiundani unavyozungumzia uzalishaji bila kuimport. Nakuambia kwa kifupi. Hii nchi gharama ya kuanzisha kiwanda ni kubwa kuliko kuagiza. . Kwa mfano ukienda china huwez kukuta kiwanda kimoja cha viatu. Unakutana na assemble center.
Unakuta kiwanda cha soli ya kiatu tu sehemu moja sehemu nyingine kiwanda cha ngoz tu nyingine kamba nyinge ulimi nk. So huyu mtu wa kuasembo anaechukua oder kwako mkishamalizana yeye sasa anacheza na hivyo viwanda tofauti tofauti kwa oder rangi na dizaini. Sasa hapa inamaanisha ukitakata kuanzisha kiwanda hapa bongo itakulazimisha kuwa na huo mlolongo wa hivyo viwanda vyote Kwa pamoja. Sasa tatizo lingine hapa kwetu ni umeme wa uhakika kodi nyingi cjui OSHA cjui nemc nk. So
Kwa mtu anaetaka hela anaangalia urahis wa kuingiza hela sio kuwa na maviwanda mengi wakati unakuwa muda mwingi unapambana na serikali. Mzee hii nchi ni ngumu kuliko unavyofikiri.
 
Kwahiyo wasikaguliwe kama wametoa RISITI??
 
Kama tunaagiza sana na kusababisha biashara kuwa nyingi basi ilitakiwa kuwe na low price kwenye hiyo biashara kwasababu ya ushindani.

Lakini pamoja na kwamba bidhaa moja kuuzwa na watu wengi tena kwenye eneo moja bado gharama zimekuwa juu.

Ushaona unaenda kuulizia bidhaa unatajiwa bei unahisi umepigwa unaondoka ukijua muhudumu atakuita m-bagain halafu unakuta muhudumu kala buyu?
 
Risiti hazitoki, na huo ndio ukweli.
 
Waachane Ni migomo ni njia ya kizamani Sana yakutatua migogoro...wakae meza moja nawahusika wayamalize.
"Ila list za kielectronic watoe waache janja janja "
Nchi hii kwa viongozi wetu hawa tulionao ni nani unayemtegemea atakuwa na time ya kukaa meza moja na wauza maduka kujadili maslahi ya wafanya biashara?

Hii kibongo bongo ipo kwenye movies tu
 

Mkuu

Kuna wafanya biashara kariakoo kwenye mfumo wa Mlipa kodi inaonekana wanaingiza Sana kupitia hapo bandarini.

Chakushangaza kwenye mfumo wa Machine VWAT hawaonekani.

Nini kinafanyika ; kinachofanyika kwa hao watajwa hiyo mizigo wanaiuzia store kwa jumla na REJAREJA.

REJAREJA kiaje; Anakuwa na meza ya umachinga mitaani NYAMWEZI au NARUNG'OMBE.

TRA inaanzisha operation kama hii kusaka wafanyabiashara wa namna hiyo. Siyo kwamba TRA haiwajui hao wafanya biashara. Inawajua vizuri Sana....

Asante!
 
Mkuu heshima kwako.

Unadhan nin kifanyike?, Kumbuka serikali haina uwezo wa kufanya biashara wala kuendesha viwanda.
Mimi nashauri wa stick kwenye msimamo wao huo huo mpaka serikali itapoamua kuwasikiliza
 
Nchi hii kwa viongozi wetu hawa tulionao ni nani unayemtegemea atakuwa na time ya kukaa meza moja na wauza maduka kujadili maslahi ya wafanya biashara?

Hii kibongo bongo ipo kwenye movies tu
Nchi ina bandari kubwa ila bidhaa hakuna ukienda Nairobi au Kampala pana zaga zama za kumwaga pana watu wanashusha Engine za magari hapo Nairobi karibu kila siku aisee wakati bongo ndio bandari tunazo za kutosha hivyo vitu vipo vichache maana TRA kila mfanyabiashara wao wanataka kumnyonya asifanye tena biashara labda awe anatoa rushwa na kukwepa kulipa kodi kwa watu walio nyooka ni ngumu kwenda nao sawa hao watu kwanza watakutengenezea mazingira magumu ili mradi tuu utoe chochote utasikia tunafanya ukaguzi wa miaka 12 iliyopita hiyo ipo Tanzania pekee ndio maana tunafanya vizuri SA na Zambia hata Malawi pia sio mbaya..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…