Wafanyabiashara Kariakoo wameiomba serikali iwaondoe raia kigeni (Wachina) wanaofanya umachinga

Wanatamaa sana hawa wafanyabiashara wa bongo. Wakipata competition wanaanza kulalamika.
 
Malighafi ni shida, mfano hebu jaribu kutengeneza sabuni au sukari mwenyewe uone gharama utakayoingia halafu uone mche mmoja au kilo ya sukari utaiuza sh? Lazima bei itakuwa juu.
Si kweli kuwa malighafi ndo tatizo,...

ebu mkumbuke Dangote na cement yake ya bei poa, nn kilimpata,?

Tatizo, kodi kubwa...upigaji mkubwa sana wa viongozi,.....
 
Kwa jinsi china, inavyotupa mikopo, nafuu, na kutujengea miundombinu, hao wa china huwezi kuwagusa,tukiwasumbua, tutaingia kwemye mtanziko wa kidiplomasia na china, na kwa ccm hii, Bora mwananchi afe,lakini sio kumsumbua mwekezaji,
Wachina,wahindi,Arabs, wanavunja sheria kibao, lakini nchi haiwezi kuwagusa,
Nakumbuka PM Majaliwa alienda kiwanda cha nguo urafiki, akakuta Hari mbaya ya kazi kwa wazawa, Mgeni analipwa 20M mzawa analipwa kama kibarua laki tatu! Akatoka povu weeee! Wapi hakuna kilichofanyika, miaka kumi imepita sasa!
 
Upo sahihi, wachina huwa wana bei nzuri kuliko wabongo na vitu vyao vina nafuu kwa quality kuliko madabwada watakayokuuzia wabongo.
 
Unajuq sheria zq uwekezaji nchini zina ruhusu kufanya kazi gani? Mgeni anapoingia nchini halafu anafanya biashara ambazo amekatazwa kisheria na zimeachwa kwa ajili ya wazawa ni uliukwaji wa sheria. serikali iko wapi?
Wazawa ni wezi, bidhaa ya kawaida wanataka faida kubwa humohumo kuna mawinga, better waendelee wachina, miafrika ni mijizi
 
Mbona wachina wanaleta unafuu wa maisha Kwa sisi wananchi wahali ya chini,au wewe ni Moja ya walanguzi wa kariakoo.
 
Unajuq sheria zq uwekezaji nchini zina ruhusu kufanya kazi gani? Mgeni anapoingia nchini halafu anafanya biashara ambazo amekatazwa kisheria na zimeachwa kwa ajili ya wazawa ni uliukwaji wa sheria. serikali iko wapi?
Hapo sijakuelewa point yako nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…