Wafanyabiashara Stendi ya Magufuli wataka mabasi yote yashushe na kupakia abiria hapo stendi ili wapate wateja

Hapo unakosea, nadhani mabasi yanaweza kushusha huko kote kakini safari ikianza lazima gari iingie stendi na ikiisha inapita stendi kabla ya kuelekea huko kwingine.
Nadhani hilo ndio la muhimu.
Na ndilo linalofanyika Sasa hivi mkuu
 
Sgr nayo iwe inafuata abiria. Mkuu utaratibu lazima uwepo na upo kila nchi. Hiyo ya mabus kufata abiria sio sahihi ni kulazimisha tu
imagine unakaa bunju ukisafiri kutokea Arusha au tanga via bagamoyo road inabid ukashushiwe Mbezi ili kumfurahisha shopkeeper wa stand kuu
hii aina ya uwazaji huwa inanishangaza sana
 
Ubungo kwa sasa ni kama hub ya mkoa wa dar,
 
Hapo umemdanganya mabasi yanapitia ndani ya stendi hasa yanayotumia njia ya chalinze.
 
Interest ya abiria au wateja ndiyo husababisha kuwe na
  • Nyumba za ibada hadi ufukwe wa Coco
  • Sheli hadi kwenye Masoko na makazi ta watu
  • Bar hadi kwenye makazi au maeneo ya shule.
  • Stendi za Mabasi kila chocho
Vitu lazima vikae kwa mpango...
Dar ni Jiji kubwa Serikali inapasa iweke stendi kubwa tatu...watu wazifuate stendi....
Aya magari ni makubwa hayatakiwi kabisa yapite kwenye njia za Tarura.
 
🤣 🤣 🤣
 
Hapo nakubaliana na wewe.
 
Kwa hiyo na ndege zifuate abiria walipo? Kuna haja gani ya kutumia pesa nyingi kujenga stendi??
NB: Arusha mbaki na stendi yenu maana tumeona hazina umhimu.
Na Kwa iyo pikipiki ziwe na stendi Yao na abiria wazifuate huko na kuangukia huko!!
Elewa kila kitu kina namna ya huduma yake. Je, ulishawai kuona ndege imepaki mtaani kwenu au popote ale nje ya airport? Na je, ulishawai kuona meli inapakia abiria magogoni zaidi ya bandarini?? Lakini maboti na mitumbwi yanashusha abiria popote kando ya bahari/ maziwa au mtoni.
Acha kasumba hizo na utaratibu huu uendelee.
 
✍️📝👍👌👏👊🤝🙏
 
Usitumie matako kufikiria...hakuna aliyesema kuwa abiria wa njiani asishushwe kabla ya basi kufika Magufuli bus terminal....kinachogusiwa hapa ni magari kugoma kupakia abiria hapo Magufuli
 
🙋‍♂️📝✍️👍👌👏👊🤝🙏
 
Hakika hata mimi nilipita stendi nilishangaa kwenye lile ghorofa wanauza andazi sh 100 alafu na chai kwenye kikombe cha plastic. Waliotokea mikoani vijijini wameelewa hii code.
Lakini DC na mbunge wake wanaweza kumaliza tatizo hili.
 
Unadanganya kwa faida ya Nani sasa, wengi tunatumia hicho kituo, Abood kwa mfano ana basi zinaanzia hapo magufuli,, ila kimsingi ya Magufuli haijai mapema kuliko Ile inayopaki Engen Ubungo, ndo maana watu wanaona ni bora kupandia basi Ubungo,.
 
🙋‍♂️📝✍️👍👌👏👊🤝🙏
 
Hassan Bomboko, Dc wa wilaya ya Ubungo aache kuhangaika na machangudoa wa Riverside na Sinza badala yake ajikite hili suala linalotokea katika kata yake ya Mbezi na ubungo.

Aamke alfajiri akafunge ofisi za haya Mabadi pale urafiki na shekilango ayaamuru yakapakie mbezi, magufuli bus terminal
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…