Mabibi na mabwana itakuwa ni kujidanganya kuwa kila kitu ni shwari pasipo kuangalia mrejesho tokea kwa wananchi.
Hivi serikali ya awamu hii inafahamu kwa nini ina mwonekano hasi?
View attachment 1667517
Hapo ni kibwagizo tu. Ila ukweli wa mambo ni kuwa uporaji wa haki na uhuru wa watu haujawahi mwacha yeyote salama.
Hivi:
Sheria hizi dhidi yetu ni hizo hizo dhidi yenu?
Sheria hizi dhidi ya magari yetu ni hizo hizo dhidi ya magari yenu?
Hospitali tunazotibiwa sisi ni hizo hizo mnazotibiwa nyie?
Juzi treni ya serikali imepata ajali, vipi lingekuwa basi la mtu binafsi?
Ama kwa hakika, 'mpendeni mchukieni, Lissu alikuwa na hoja."
Huu ndiyo ulio ukweli mchungu.