Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

View attachment 2657297

Shida ya watu kama nyie ni kukariri mambo hilo ni moja ya soko maarufu mjini Hong-Kong hilo eneo per square meter ni most expensive duniani. Sio mbali na hayo majengo ni downtown yao sasa yanafania ni vitu vilivyoangushwa maeneo ya Financial sector huko kwao.

Hivi unadhani capital city ya safe heaven as well as legit Financial services ina shortage ya mitaji ya kuvunja hizo dilapidated properties za street markets. Wanayaacha kwa sababu ya kulinda identity ya eneo na tamaduni za watu wao.

Sisi badala ya kutaka kuona kariakoo tunaondoa vibaka iwe sehemu salama ya watalii kuweza kuja kununua vitu vya kitanzania; kama kwingine duniani tunataka kuibadilisha.

Nimekuwekea na article ya kwanini giants supermarkets za west nyingi zilishindwa mainland China; kwanza upewi eneo la uwekezaji wa retail karibu na popular street markets ili kulinda long customs zao.

Embu waafrica acheni ushamba wa kudhani kila kitu lazima kibadilike.

Ukirudi huko kwenye huo mkataba unaotetea subiri hao wafanyabiashara waende mahakamani halafu mkataba udadavuliwe kwa terms z commercially contracts. Ndio utaelewa kwa hiyo notice waliyotoa NHC lazima walipe fidia ni mda mdogo mno; hapo watu wanahitaji si chini ya miaka miwili kuwatoa wenye maduka yao.

Mnatoa mambo vichwani mwenu tu na kubwabwaja as if kwenye hii dunia hakuna kanuni za kuishi na kufanya mambo.
Kariakoo kuna utamaduni gani ambao NHC wanatakiwa kuulinda?
Yani shirika lipo kwenye real estate na housing unalitaka lifanye mambo ya utamaduni. Hiyo sio Kilwa, Bagamoyo wala mji mkongwe Zanzibar.
Hiyo ni business hub tunategemea Wakongo, Wazambia, Wanyarwanda, Warundi na wengine waje kufanya biashara tukuze uchumi, hayo majengo yaboreshwe. Huwezi yatumia makumi ya miaka mpaka yaanze kuporomoka na kuua.

Huwezi enda Manhattan na njaa za usiku mmoja ukasema wasibomoe jengo la kizee kujenga jengo kubwa na bora kwa kudai utakula wapi. Hiyo Hong Kong unayoleta kwenye article huwa hawabomoi majengo ya zamani? Au skyscrapers zote zile zilijengwa kwenye pori.
 
kwani mtaani hakuna nyumba zingine za kupanga, hivi hao jamaa mbona wamelemaa sana akili zao? hapo NHC si wanapanga, waondoke na pango ambalo wangelipa hapo wakalipe mtaani, mwenye nyumba ni mfanyabiashara anataka kuboresha nyumba zake. au wanaamini hizo nyumba walipewa ni zao? pimbi kabisa hawa.
 
Kariakoo kuna utamaduni gani ambao NHC wanatakiwa kuulinda?
Yani shirika lipo kwenye real estate na housing unalitaka lifanye mambo ya utamaduni. Hiyo sio Kilwa, Bagamoyo wala mji mkongwe Zanzibar.
Hiyo ni business hub tunategemea Wakongo, Wazambia, Wanyarwanda, Warundi na wengine waje kufanya biashara tukuze uchumi, hayo majengo yaboreshwe. Huwezi yatumia makumi ya miaka mpaka yaanze kuporomoka na kuua.

Huwezi enda Manhattan na njaa za usiku mmoja ukasema wasibomoe jengo la kizee kujenga jengo kubwa na bora kwa kudai utakula wapi. Hiyo Hong Kong unayoleta kwenye article huwa hawabomoi majengo ya zamani? Au skyscrapers zote zile zilijengwa kwenye pori.
Inaonekana neno ‘heritage’ halipo kwenye vocabulary yako.

Sio China na Hong tu karibu kila nchi iliyoendelea ina masoko ambayo yapo prime areas na mwonekane wake umepitwa na wakati; investors wangependa kuyavunja lakini yanaachwa kwa sababu ni local heritage.

3933F7CB-BBAF-4AB2-BB48-D8843DB6EA4F.jpeg

7A0A1254-12DC-4A45-B8B8-85A27BCFA980.jpeg

Hiyo sehemu inaitwa Notting Hill ni karibu sana na mjini kabisa London westend.

Halafu hiyo Portobello ebu ingia google angalia bei za nyumba hapo.

Hiko kiduka cha nguo mtu akiuza si £1 million na ukitengeneza baada ya hapo ikawa apartment si chini ya £1.5 hivyo viduka unavyoviona vimetundika nguo na mazaga zaga.

Halafu huko ndio wanaishi A list stars na matajiri wengine. Lakini maeneo hayo pia kuna nyumba za serikali, masoko kama hayo na hiyo barabara ni protected by law kwa sababu ni heritage area; ukiuza duka anaenunua hapo awezi kugeuza hiyo sehemu vinginevyo atalitumia kama duka tu.

Embu acheni hizo akili za kufikiria kubomoa kila kitu; si wajenge maeneo mengine sio kupenda cheap returns tu.
 
Kariakoo kuna utamaduni gani ambao NHC wanatakiwa kuulinda?
Yani shirika lipo kwenye real estate na housing unalitaka lifanye mambo ya utamaduni. Hiyo sio Kilwa, Bagamoyo wala mji mkongwe Zanzibar.
Hiyo ni business hub tunategemea Wakongo, Wazambia, Wanyarwanda, Warundi na wengine waje kufanya biashara tukuze uchumi, hayo majengo yaboreshwe. Huwezi yatumia makumi ya miaka mpaka yaanze kuporomoka na kuua.

Huwezi enda Manhattan na njaa za usiku mmoja ukasema wasibomoe jengo la kizee kujenga jengo kubwa na bora kwa kudai utakula wapi. Hiyo Hong Kong unayoleta kwenye article huwa hawabomoi majengo ya zamani? Au skyscrapers zote zile zilijengwa kwenye pori.
Leo unashusha Darasa tu kaka.
 
Wafanyabiashara wa maduka kutoka soko la Kariakoo wamefika makao makuu na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupinga notice walizopewa na shirika hilo kwa kuwataka kuhama ndani ya siku 90 kupisha mwekezaji mpya katika eneo hilo.

Wafanyabiashara hao wamesema, wao hawapingi maendeleo lakini muda uliotolewa na NHC ni mfupi sana na wamemuomba Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuingilia kati sakata hilo ili waweze kupata haki yao kwani muda waliopewa ni mfupi sana kwa wao kuhama kutokana wao kuwa na madeni na mikopo.

====

View attachment 2657014
NOTISI YA SIKU TISINI (90) YA KUSITISHA MKATABA WA UPANGAJI WA NYUMBA NA 005 KWENYE KIWANJA NA 23 KITALU NA 31 MTAA WA TANDAMTI NA SWAHILI

Tafadhali husika na somo hapo juu;

Unafahamishwa kuwa Shirika la Nyumba la Taifa limeanza rasmi utekelezaji wa Sera va Ubia na wawekezaji binafsi na taasisi mbalimbali ambayo ilizinduliwa rasmi mwezi Novemba 2022.

Hivyo basi Shirika la Nyumba la Taifa lina mpango wa kuanza ujenzi kwenye Kiwanja tajwa hapo juu ambapo wewe ni mpangaji, hivyo tunakutaarifu kwamba unapewa NOTISI ya siku tisini (90) kuanzia tarche 02/06/2023 mpaka tarehe 31/08/2023 kusitisha mkataba baina yako na Shirika la Nyumba la Taifa kwenye nyumba tajwa hapo juu.

Shirika limerejea kipengele namba 4.1 (c). (d) na 7.2 cha Mkataba wa Upangaji kinachompa mamlaka mpangishaji kuvunja mkataba ndani ya siku tisini (90) pale anapohitaji jengo lake kwa ajili ya matumizi mengine.

Kwa maelezo hayo, unapewa NOTISI ya siku tisini (90) ya kutakiwa kuhama katika nyumba unavoishi ili kupisha uendelezaji unaokusudiwa kufanyika katika kiwanja hicho.

Unaruhusiwa kuomba upangaji upya baada ya jengo jipya kukamilika kulingana na masharti ya kipindi hicho.

Pia soma: Wapangaji nyumba za NHC Kariakoo walalamika notisi za kuhama bila mazungumzo, wadai NHC wamempa dili mwekezaji mpya kimyakimya
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka
 
Inaonekana neno ‘heritage’ halipo kwenye vocabulary yako.

Sio China na Hong tu karibu kila nchi iliyoendelea ina masoko ambayo yapo prime areas na mwonekane wake umepitwa na wakati; investors wangependa kuyavunja lakini yanaachwa kwa sababu ni local heritage.

View attachment 2657462

View attachment 2657483

Hiyo sehemu inaitwa Notting Hill ni karibu sana na mjini kabisa London westend.

Halafu hiyo Portobello ebu ingia google angalia bei za nyumba hapo.

Hiko kiduka cha nguo mtu akiuza si £1 million na ukitengeneza baada ya hapo ikawa apartment si chini ya £1.5 hivyo viduka unavyoviona vimetundika nguo na mazaga zaga.

Halafu huko ndio wanaishi A list stars na matajiri wengine. Lakini maeneo hayo pia kuna nyumba za serikali, masoko kama hayo na hiyo barabara ni protected by law kwa sababu ni heritage area; ukiuza duka anaenunua hapo awezi kugeuza hiyo sehemu vinginevyo atalitumia kama duka tu.

Embu acheni hizo akili za kufikiria kubomoa kila kitu; si wajenge maeneo mengine sio kupenda cheap returns tu.
Nimekuuliza kuna heritage gani Kariakoo au zile nyumba nyingine zina nyufa, rangi imepauka, zimekarabatiwa zimerudiwa simenti, zinavuja mvua ikinyesha na mifumo ya umeme inasumbua ndio unaita heritage. Vitu vichafu ndio unataka viwe heritage.

Heritages za Dar zilijulikana vitu kama msikiti wa Kwamtoro, ikulu ya Magogoni, ukumbi wa Anatouglou, Karimjee na vitu kama hivyo. Sio fremu za maduka zilizochakaa. Yakibomoka au yakiungua watayaacha magofu?
 
Wawalipe fidia za loss of income kwa miaka kadhaa ndio watu wanavyofanya na gharama fixtures and fittings za maduka yao; sio kupenda mambo rahisi.

Yaani unachukulia poa tu kisa jengo mali yako utadhani watu awakutafuta hizo hela za kuwekeza hapo.
Kama mkataba unaeleza hivyo, itabidi waharakishiwe malipo yao kabla hawajaondoka.
 
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka
somo ni kubwa. halafu kila mwezi analipa kodi hapo, si ahamishe tu ile kodi akalipe mtaani, na amepewa notice ya miezi mitatu mizima. yeye analia anasema samia tusaidie tutaenda wapi? nenda kapange mtaani ndio tunataka uende. wanatakiwa kujua kuwa hizo nyumba ni shirika la serikali, ni nyumba za watanzania wote. hata sisi ambao hatujawahi kuzikaaa ni za kwetu.
 
Na bado,ipo siku mtahamishwa dar muende nje ya mji huko Kiromo,Pinga,Mabwepande,Kibaha ndani huko
 
Kuna watu huwa wanajifanya vichwa ngumu

Hiyo ni official note ila kuna informal note ilishatolewa nadhani toka mwezi wa kwanza

Lakini bado kuna watu wakalipia Kodi ya mwaka
 
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka

Hebu mkuu tuonyeshe hati ya kakiwanja kako hapo kariakoo
 
Kuna watu huwa wanajifanya vichwa ngumu

Hiyo ni official note ila kuna informal note ilishatolewa nadhani toka mwezi wa kwanza

Lakini bado kuna watu wakalipia Kodi ya mwaka
Sasa kodi walilipa kwa nani?
Au ndo wanaotembeza vinote kuwa washalipa?

Maana hadi maeneo ya Fire wameambiwa wasilipe kodi wajiandae
 
Katika hili nadhani serikali itumie tu busara na huruma kwa kuwapa hata notisi ya mwaka mmoja wahame. Wafanyabiashara wengi wana mikopo ambayo hadi wauze ndo wapate rejesho. Katika huo mwaka wanaweza kujiandaa na kuwapanga wateja wao waende kwenye ofisi zao zingine. Kwa upande mwingine ni funzo kwa wafanyabiashara vilaza wanaodharau elimu na kudhani ukiwa na hela ndo kila kitu. Serikali hapo ikiamua isisikilize mtu tayari hao jamaa ni kilio kwasababu NHC kisheria wako sawa.
Umewahi ona wapi notisi ya mwaka 1?
 
Back
Top Bottom