Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Kariakoo kuna utamaduni gani ambao NHC wanatakiwa kuulinda?
Yani shirika lipo kwenye real estate na housing unalitaka lifanye mambo ya utamaduni. Hiyo sio Kilwa, Bagamoyo wala mji mkongwe Zanzibar.
Hiyo ni business hub tunategemea Wakongo, Wazambia, Wanyarwanda, Warundi na wengine waje kufanya biashara tukuze uchumi, hayo majengo yaboreshwe. Huwezi yatumia makumi ya miaka mpaka yaanze kuporomoka na kuua.

Huwezi enda Manhattan na njaa za usiku mmoja ukasema wasibomoe jengo la kizee kujenga jengo kubwa na bora kwa kudai utakula wapi. Hiyo Hong Kong unayoleta kwenye article huwa hawabomoi majengo ya zamani? Au skyscrapers zote zile zilijengwa kwenye pori.
 
kwani mtaani hakuna nyumba zingine za kupanga, hivi hao jamaa mbona wamelemaa sana akili zao? hapo NHC si wanapanga, waondoke na pango ambalo wangelipa hapo wakalipe mtaani, mwenye nyumba ni mfanyabiashara anataka kuboresha nyumba zake. au wanaamini hizo nyumba walipewa ni zao? pimbi kabisa hawa.
 
Inaonekana neno ‘heritage’ halipo kwenye vocabulary yako.

Sio China na Hong tu karibu kila nchi iliyoendelea ina masoko ambayo yapo prime areas na mwonekane wake umepitwa na wakati; investors wangependa kuyavunja lakini yanaachwa kwa sababu ni local heritage.





Hiyo sehemu inaitwa Notting Hill ni karibu sana na mjini kabisa London westend.

Halafu hiyo Portobello ebu ingia google angalia bei za nyumba hapo.

Hiko kiduka cha nguo mtu akiuza si £1 million na ukitengeneza baada ya hapo ikawa apartment si chini ya £1.5 hivyo viduka unavyoviona vimetundika nguo na mazaga zaga.

Halafu huko ndio wanaishi A list stars na matajiri wengine. Lakini maeneo hayo pia kuna nyumba za serikali, masoko kama hayo na hiyo barabara ni protected by law kwa sababu ni heritage area; ukiuza duka anaenunua hapo awezi kugeuza hiyo sehemu vinginevyo atalitumia kama duka tu.

Embu acheni hizo akili za kufikiria kubomoa kila kitu; si wajenge maeneo mengine sio kupenda cheap returns tu.
 
Leo unashusha Darasa tu kaka.
 
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka
 
Nimekuuliza kuna heritage gani Kariakoo au zile nyumba nyingine zina nyufa, rangi imepauka, zimekarabatiwa zimerudiwa simenti, zinavuja mvua ikinyesha na mifumo ya umeme inasumbua ndio unaita heritage. Vitu vichafu ndio unataka viwe heritage.

Heritages za Dar zilijulikana vitu kama msikiti wa Kwamtoro, ikulu ya Magogoni, ukumbi wa Anatouglou, Karimjee na vitu kama hivyo. Sio fremu za maduka zilizochakaa. Yakibomoka au yakiungua watayaacha magofu?
 
Wawalipe fidia za loss of income kwa miaka kadhaa ndio watu wanavyofanya na gharama fixtures and fittings za maduka yao; sio kupenda mambo rahisi.

Yaani unachukulia poa tu kisa jengo mali yako utadhani watu awakutafuta hizo hela za kuwekeza hapo.
Kama mkataba unaeleza hivyo, itabidi waharakishiwe malipo yao kabla hawajaondoka.
 
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka
somo ni kubwa. halafu kila mwezi analipa kodi hapo, si ahamishe tu ile kodi akalipe mtaani, na amepewa notice ya miezi mitatu mizima. yeye analia anasema samia tusaidie tutaenda wapi? nenda kapange mtaani ndio tunataka uende. wanatakiwa kujua kuwa hizo nyumba ni shirika la serikali, ni nyumba za watanzania wote. hata sisi ambao hatujawahi kuzikaaa ni za kwetu.
 
Na bado,ipo siku mtahamishwa dar muende nje ya mji huko Kiromo,Pinga,Mabwepande,Kibaha ndani huko
 
Kuna watu huwa wanajifanya vichwa ngumu

Hiyo ni official note ila kuna informal note ilishatolewa nadhani toka mwezi wa kwanza

Lakini bado kuna watu wakalipia Kodi ya mwaka
 
Kuna SoMo lakujifunza je nikweli mtu ako nyumba ya nhc miaka yote hujatafuta Kiwanja ukajenga upo kwa watu? Huu ni umasikini mwingine. Nyumba ya nhc sio nyumba yako binafsi so waheshim mamlaka

Hebu mkuu tuonyeshe hati ya kakiwanja kako hapo kariakoo
 
Kuna watu huwa wanajifanya vichwa ngumu

Hiyo ni official note ila kuna informal note ilishatolewa nadhani toka mwezi wa kwanza

Lakini bado kuna watu wakalipia Kodi ya mwaka
Sasa kodi walilipa kwa nani?
Au ndo wanaotembeza vinote kuwa washalipa?

Maana hadi maeneo ya Fire wameambiwa wasilipe kodi wajiandae
 
Umewahi ona wapi notisi ya mwaka 1?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…