Kwanini uvunje investments ambazo ni cashcows za shirika kisa tu ni prime area. Badala ya kutafuta maeneo ya wazi utanue jiji kama una hiyo mitaji.
Hizo ndio akili za investment za watanzania kupenda mambo rahisi. Serikali imewapa hela ya kumaliza mradi wao wa Kinondoni na Kawe apartments; kwanini wasisubiri iishe wapime occupancy rates ya hiyo miradi kabla ya kuruhusu upuuzi mwingine.
Ni mipango ya ovyo mno; kwa sasa NHC inapata 100% revenue ya hayo majengo, si ajabu baada ya uwekezaji wa ubia kila kitu kikikiisha mapato yakawa chini baada ya kukagawana na mwekezaji.
Hakuna la maana hapo zaidi ya uwekezaji, halafu kuondoa biashara 1000 ambazo zinalipa kodi kiasi gani unapoteza serikali, kiasi gani cha hasara unaweza zipa Bank, familia ngapi unazipa umaskini.
Huyu mama anachezewa sana na mafisadi, 2025 nyumba yake ya uraisi anayostahili kujengewa na serikali huko Kizimkazi au popote alipochahua tuakikishe ishaisha; hiyo kazi sio ya size ata kidogo tunalazimisha tu.