Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Wafanyabiashara wa Kariakoo wagoma kuhama kupisha Wawekezaji

Kwa hio Majengo ya NHC makuuu kuu toka mwaka 50 yaachwe, Jengo lina Frame 3 liachwe wakati linaweza bomolewa na kuwekwa Frame 72 na Appaetment 40? Zitakazoingiza Takriban Bilioni kwa mwaka badala ya milioni 2?

Kama huoni hii opportunity Kariakoo haikuhusu, ni eneo la Biashara lile wanatakiwa watu wanaofikiria kibiashara ndio wafanye Decisions, hata hao wanaolalamika kutolewa wanaomba tu Extension ya Muda kuonesha na wao wanafikiri kibiashara.

Na biashara haifati majengo kamwe, Majengo ndio hufuata biashara, mpaka kesho Machinga Complex pamedoda, unafikiri Serikali ikijenga majengo Nje ya Kkoo basi kutachangamka na kua na Biashara?
Kwa sasa Kariakoo majengo mengi yanavunjwa na kuongezewa uwezo wa kuchukua watu wengi zaidi, pamoja na stoo na makazi. Hii inasaidia mambo mengi sana.

Hapo alipo Tahfif uhakika halipi kodi ya milioni kwa mwezi
 
Yawezekana ni Mimi sijui, ila ukweli ni kuwa 90 days is way overdue... Huko kwingine unakokusema hakuna mahali wazaidisha 60 days.

Pili NHC ni landlord kama wewe na Mimi tunapopangisha ndio maana anakwenda kwa kufuata sheria, Swala la biashara yako na wewe kukaa sana kwangu havina uhusiano na property yangu, ndio maana makampuni makubwa yanajenga ofisi au yanaingia kwenye makubaliano ya long term lease.

Yaani unilipe kila mwezi halafu uniambie nikikutoa nakuharibia biashara, ungejua Hilo ungekuja mezani ukaniambia nataka kukaa hapa at least kwa miaka 10 ningekupa my stance, pay me this much au hapana tafuta kwingine natarajia.kuvunja in 6 years.

Shida yetu tunapenda sana kuoperate kila kitu kwa the exception rule. Hapana sio sahihi.
Public housing ni different rules nchi nyingi uwezi mtoa mpangaji kabisa labda awe halipi kodi.

Halafu schemes nyingi sio zote huwa buy to let, lakini swala la kutoana kama NHC huwa halipo.

Kwa hivyo if you are gonna do it, hakikisha zoezi ni responsible.

Siku tisini sio nyingi kwa upande for residential properties walau miezi sita ya rent free.

Kwa wafanyabiashara ni definitely ndogo kwa sababu wana financial obligation kadhaa kwenye hizo biashara, bila ya compensation ni mpaka mkataba rasmi una expire au unalipa fidia.

Niko barabarani for my walks na sina miwani ata ku type shida.

Usiku mwema

👋
 
Kuna jamaa mmoja aliwahi kuja humu kuomba ushauri, kwamba baba yake anataka amtafutie kazi ya jeshi, lakini mtoto anataka kufanya biashara. Baba mtu alimuambia biashara za Tanzania hazitabiriki.

Chukulia mfano umekopa benk umewekeza kwenye biashara ya duka halafu unaambiwa uhame.

Ndio maana viongozi wanapambana watoto wao waajiriwe kwenye vitengo vyenye mishahara mikubwa na marupurupu mana kuna uhakika kuliko biasharani kwa hapa TZ.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Kwanini uvunje investments ambazo ni cashcows za shirika kisa tu ni prime area. Badala ya kutafuta maeneo ya wazi utanue jiji kama una hiyo mitaji.

Hizo ndio akili za investment za watanzania kupenda mambo rahisi. Serikali imewapa hela ya kumaliza mradi wao wa Kinondoni na Kawe apartments; kwanini wasisubiri iishe wapime occupancy rates ya hiyo miradi kabla ya kuruhusu upuuzi mwingine.

Ni mipango ya ovyo mno; kwa sasa NHC inapata 100% revenue ya hayo majengo, si ajabu baada ya uwekezaji wa ubia kila kitu kikikiisha mapato yakawa chini baada ya kukagawana na mwekezaji.

Hakuna la maana hapo zaidi ya uwekezaji, halafu kuondoa biashara 1000 ambazo zinalipa kodi kiasi gani unapoteza serikali, kiasi gani cha hasara unaweza zipa Bank, familia ngapi unazipa umaskini.

Huyu mama anachezewa sana na mafisadi, 2025 nyumba yake ya uraisi anayostahili kujengewa na serikali huko Kizimkazi au popote alipochahua tuakikishe ishaisha; hiyo kazi sio ya size ata kidogo tunalazimisha tu.
Umesikia Dar Kuna shida ya frame za biashara!? Hao Watu ni ving'ang'anizi na siku zote hukwamisha maendeleo, unakuta mtu analipwa fidia halafu kuhama hataki!! Ndio watu WA Dar, hakuna kudekezwa!!
 
Public housing ni different rules nchi nyingi uwezi mtoa mpangaji kabisa labda awe halipi kodi.

Halafu schemes nyingi sio zote huwa buy to let, lakini swala la kutoana kama NHC huwa halipo.

Kwa hivyo if you are gonna do it, hakikisha zoezi ni responsible.

Siku tisini sio nyingi kwa upande for residential properties walau miezi sita ya rent free.

Kwa wafanyabiashara ni definitely ndogo kwa sababu wana financial obligation kadhaa kwenye hizo biashara, bila ya compensation ni mpaka mkataba rasmi una expire au unalipa fidia.

Niko barabarani for my walks na sina miwani ata ku type shida.

Usiku mwema

👋
Anatakiwa ahamishe biashara yake na pindi jengo likikamilika akubaliane na masharti mapya
 
Kuna jamaa mmoja aliwahi kuja humu kuomba ushauri, kwamba baba yake anataka amtafutie kazi ya jeshi, lakini mtoto anataka kufanya biashara. Baba mtu alimuambia biashara za Tanzania hazitabiriki.

Chukulia mfano umekopa benk umewekeza kwenye biashara ya duka halafu unaambiwa uhame.

Ndio maana viongozi wanapambana watoto wao waajiriwe kwenye vitengo vyenye mishahara mikubwa na marupurupu mana kuna uhakika kuliko biasharani kwa hapa TZ.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Mkopo si unawekeza kwenye Mtaji? NHC hawachukui mtaji wa mtu.

Na pia hakuna mfanyabiashara mpya anayeanza awe na frame NHC, kule kuna mapapa ambao wameanza biashara miaka 30 ama 40 iliopita ama mtu mwenye Mtaji mkubwa na anaweza lipa kilemba milioni 10-70.

Wengi wanalia hapo ni vilemba ama wameingizwa mjini. Watu walishajua haya majengo yanakuja Kubomolewa wakauza frame, mtu katoa milioni 70 yake hapo hata mwaka haujaisha kapewa Notice unategemea awe na hali gani?
 
Naona kama wameadhibiwa wale kwasababu ya ule mgomo, sitegemei hao jamaa waje kupangishwa tena kwenye hayo majengo mbele ya safari, ndio wameshaondolewa kijanja hivyo.

Ngoja tuone kama kweli huo mradi mpya utaanza hivi karibuni, au ndio kwasababu wameshapata sababu ya kuwaondoa hao jamaa, basi na mambo mengine yatalala.
Nhc walisema wanataka kujenga skyscraper 19 eneo la kariako Naona ndio wameanza mikakati .
Miezi 3 ni mingi wajipange kuondoka maeneo ya kuishi ni mengi !
 
Nhc walisema wanataka kujenga skyscraper 19 eneo la kariako Naona ndio wameanza mikakati .
Miezi 3 ni mingi wajipange kuondoka maeneo ya kuishi ni mengi !
Kwanza Kwa Sasa huko kariakoo huwezi kwenda na Gari, hakupitiki, mtu ukisikia maboresho unasema Mungu kawaona Hawa Watu, Hawa wanaoandamana ni WA kupuuzwa Kwani ni wapinga maendeleo,
 
huyo mama anasema ana miaka 60 kwenye nyumba za NHC, miaka yote hajawapa watanzania wenzake wapange, na bado analeta jeuri anaamini hapo ni nyumbani kwake. sweken kabisa. anasema anaonewa, anasema ataenda wapi akifukuzwa, miaka 60 ameishi hapo hadi ameona kama ni kwake. NHC ijifunze, isipangishe mtu mmoja miaka yote hiyo, wanasahau kujenga na wanaamini hapo ndio wamefika ni pao.
Ukiangalia miaka 60 maana yake tangu Dar ikiwa inaishia magomeni na viwanja vilikuwa bei ya Chini Sana, sasa mji unakua yeye anaangalia tu hajengi nyumba ya kwake Leo analalamika kuondolewa kwenye nyumba ya kupanga.
 
Kuna jamaa mmoja aliwahi kuja humu kuomba ushauri, kwamba baba yake anataka amtafutie kazi ya jeshi, lakini mtoto anataka kufanya biashara. Baba mtu alimuambia biashara za Tanzania hazitabiriki.

Chukulia mfano umekopa benk umewekeza kwenye biashara ya duka halafu unaambiwa uhame.

Ndio maana viongozi wanapambana watoto wao waajiriwe kwenye vitengo vyenye mishahara mikubwa na marupurupu mana kuna uhakika kuliko biasharani kwa hapa TZ.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
Walipewa taarifa toka Mwezi wa Kwamza kuwa kodi haitapokelewa, hivyo wengi wamekuwa wakiishi bure.
 
Niliwahi sikia kuwa hizi nyumba zilikuwa za wakoloni na serikali ilizitaifisha na kuwa zao na wengine wanaoishi katika nyumba hizo kama wapangaji zilikuwa ni nyumba za baba au Babu zao.

Hoja ni kwamba tayari nyumba ziko katika mikono ya serikali na hili linafahamika hivyo. Sasa serikali kupitia Shirika la nyumba wametoa notisi ilii waondoke ilii nyumba zikarabatiwe au zijengwe upya kisasa zaidi ka dhana ya kuendelea mji wao hawataki kutoka, hii sioni kama ni sawaa inabd wapishe ujenzi ufanyike na pengine zitajengwa ndefuu zaidi ili kuongeza idadi ya wapangaji wa makazi na maduka kitu ambacho ni kizuri.

Ninachoshauri hawa watu wapishe ujenzi ila wawekwe kwenye orodha ya wapangaji. Ambapo pindi ujenzi ukikamilka watapata kipaumbele cha kupangishwa

Ahsanteni sanaa, sio kila kitu ni siasa.
 
Hakuna ulijuwalo, kuna majengo wamiliki wa zamani walipewa floor kadhaa.

Ikitokea kuna uwekezaji lazima kuwe na MoU ujenzi ukikamilika watapewa floor ngapi.
 
Hakuna ulijuwalo, kuna majengo wamiliki wa zamani walipewa floor kadhaa.

Ikitokea kuna uwekezaji lazima kuwe na MoU ujenzi ukikamilika watapewa floor ngapi.
Je ni wote walipewa hizo floor? Unataka katikati ya mji yabaki majengo ya miaka ya 1930? Je unafikilia uwekezaji ukifanyika watakosa hiyo haki ?zile nyumba inabd zivunjwe yapande magorofa yenye hadhi ya kariakoo kama kitovu Cha jiji
Hii Tabia ya kumvimbia mwenye nyumba na ww ni mpangaji huo ujasiri wanautoa wapi ? Na wamepewa notsi Kwa kufuata utaratibu wa mkataba wa upangaji shida iko wapi
 
Hakuna ulijuwalo, kuna majengo wamiliki wa zamani walipewa floor kadhaa.

Ikitokea kuna uwekezaji lazima kuwe na MoU ujenzi ukikamilika watapewa floor ngapi.
We jamaa unapenda ligi na siasa sana.
 
Mkopo si unawekeza kwenye Mtaji? NHC hawachukui mtaji wa mtu.

Na pia hakuna mfanyabiashara mpya anayeanza awe na frame NHC, kule kuna mapapa ambao wameanza biashara miaka 30 ama 40 iliopita ama mtu mwenye Mtaji mkubwa na anaweza lipa kilemba milioni 10-70.

Wengi wanalia hapo ni vilemba ama wameingizwa mjini. Watu walishajua haya majengo yanakuja Kubomolewa wakauza frame, mtu katoa milioni 70 yake hapo hata mwaka haujaisha kapewa Notice unategemea awe na hali gani?
Hatari sana! Pole yao.

Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom