Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

1:Wapi nitapata Madera ya kisomali kwa Bei ya jumla?
2: Vijora vya Mombasa nikiamua kuvifata hukohuko Mombasa si ndo vizuri au Mombasa Ni jina tu?
3:Mashati ya kiume jamaa naona wanauza jumla 11000 je wao wanachukua wapi na kwa shngapi?
Hii Msomali Mi nanunuliaga mtaa wa Congo na Aggrey, ukiwa uhuru unaingilia kwenye kile kiuchochoro flan hivi cha vumbi ambacho mdawote kipo nyomii,

Wengi ni wahindi, na bei zao ni elf 23, hata juzi tuu nimechukua,

Kuhusu shati Mimi kuna sehemu hio hio congo na agrey nachukuaga kwa 7000-8000 ila hua mzigo wake ni Mdogo mwishowe naenda kwa hawa wa 11,000,

Bado nasaka hilo chimbo,
Vipi jeans kuna sehemu unapata bei nzuri?

Kuna baharia alishawahi niuzia shati hizi za 12 kwa elf 6 na jeans za 13 kwa elf 8, Nilinunua haraka Nikiamini alikosea.
Yule jama sijawahi mpata tena, lile duka asaivi sio yeye.
 
Wadau kwa anaejua chimbo la chupi za watoto na vest naomba mnijuze tafadhali
 
Jaman Natafuta Connection ya SOKO la maharage ya bukoba dar...Nina maharage ya njano gunia kadhaa...kilo nauza 2,300 kwa jumla

0744277050
 
Ukipata unijuze kak
Jeans huwa zipo underground moja hivi ila zinakuja chache hivyo wale jamaa wanawajulisha wateja wao(wenye maduka nje ya Kariakoo)

Mzigo ukifunguliwa wanazivamia zinaisha au zinabakia chache
Wale wa rejareja wanabakia kuuziwa Midosho
 
Jeans bado pia nazisaka....Hawa wanaotuuzia vijora,mashati na jeans mzigo wanatoa wapi aisee au ndo wanaagiza nje?
 
Kiatu kinauzwa laki lakini ukifuatilia unaambiwa ukijua chimbo unaweza kupata 20000 siku ya kufungua.

Shati Kali unique Nyumba classic ambayo Dukani hata 50000 inauzwa lakini nasikia ukijua chimbo hata 10000 unachukua.

Kadeti za maana. Mwenge 50,000 -60000 lkn ukifuatilia unakuta chimbo hata 12000.

Wakuu wazee wa Machimbo, wazee wachocho wale wanaomini unaweza kuwa mtanashati kitu hadi shati kwa chini ya 59K. Wakati unapishana na watu wakiwa na products hizo hizo lakini imewacost zaidi ya 300K.

Karibuni sio biashara. Utanashati. Utanashati huficha umasikini, lakini pia unaweza kuingia dili kubwakubwa na watu wa maana ka jinsi unavyyonekana na unavyojiweka.
 
KWA WAMILIKI WA MADUKA
Je! unamiliki biashara ndogo na unapata changamoto katika upigaji hesabu?
suluhisho tunalo, huduma utakazozipata.
1) ukaguzi wa hesabu za biashara
2) hesabu za faida au hasara
3) ushauri
n.k
GHARAMA NI NDOGO
 
Inategemea na ushamba wako, shati unanunua sh.ngapi ??

Labda wewe niwakuja mjini... Unaamin vitu vinanunuliwa hussein pamba kali tu
Unadanganya wenzanko, hakuna shati la ukweli chini ya 20,000/= inategemea labda wewe shati kali kwako ni lipi, hata 2000 unapata.
 
Inategemea na ushamba wako, shati unanunua sh.ngapi ??

Labda wewe niwakuja mjini... Unaamin vitu vinanunuliwa hussein pamba kali tu
Mimi nimezaliwa Dar, nipo mji huu tangu ukiitwa mzizima.

Hapo mtaa wa Congo wamachinga walikuwa wakiuza samaki sangara na siyo mitumba.

Wengi tulikuwa mitaa hiyo tunakuja kula pilau kwa Bamchawi au Red star mtaa wa Congo.

Sh 8000 utauziwa matambala na siyo shati.

Toyota Starlet na Toyota IST yote ni magari, lakini anayejuwa gari na catalogue atajuwa hapo achukuwe gari gani.
 
Nimeona ikabidi ninyamaze[emoji16]
 
Mimi naomba msaada anaejua suppliers wa vifaa vya kupikia na kupambia keki na mapambo ya sherehe kwa jumla.
Thanks in Advance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…