Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wakuu.. msaada wa chimbo naloweza kupata sandles/ flip flops za kiuke kwa bei ya jumla...
ukiweka na bei itapendeza sana..

asanteni
 
Unatumia jina gani Insta?? Na shati walau standard quality inaanzia bei gani???
 
Wakuu mimi naomba connection ya mtu anae uza makufuli kwa bei ya chini hapo K/Koo
 
Naomba mwenye kufahamu wapi naweza kupata vitambaa vya sofá ama makochi hapo kariakoo naomba mawasiliano nitamtuma mtu.
 
Anayejua chimbo la kununua dawa za binadamu kwa jumla anicheki 0788364580
 
Naomba mwenye kufahamu wapi naweza kupata vitambaa vya sofá ama makochi hapo kariakoo naomba mawasiliano nitamtuma mtu.

Gerezani na bei nafuu mno hadi utashangaa
Ila zunguka maduka tofauti tofauti kabla ya kufanya manunuzi
 
nataka jiko la gesi plate gas na umeme plate 1 oven itumie umeme mwenye chimbo anisaidie bei iwe nzur kampuni nzuri pia
 
Gerezani na bei nafuu mno hadi utashangaa
Ila zunguka maduka tofauti tofauti kabla ya kufanya manunuzi
Mkuu kuhusu nguo za ndani nilienda ile mitaa yake pale Kariakoo ila bei ilikuwa kubwa kuliko bei ya Mbeya ambako ndio nilitaka nitume baadhi ya mzigo. Nilikata tamaa maana nilienda kama mara tatu kutafuta bei nafuu ila wote bei zilezile
 
Maybe maduka ya mwanzoni ila ya ndani ndani mengi bei nafuu japo sasahivi bidhaa nyingi zimepanda kiasi
 
Maybe maduka ya mwanzoni ila ya ndani ndani mengi bei nafuu japo sasahivi bidhaa nyingi zimepanda kiasi
Tangu January bidhaa zilipanda bei. Bei niliyouliza December mwishoni siyo niliyoikuta January baada ya kodi kuchachamaa
 
Naombeni kujuzwa chimbo la

-Vitambaa vya kushona jumla (vya kike)
-Vijora jumla
-madera ya bei za jumla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…