Naona uzi umepoa. Ngoja nishushe vitu.
.
Unataka Kufanya Biashara ya Vyombo vya plastiki kama viti, meza, vikombe, majagi, mabeseni nk. maduka ya viwanda yapo kariakoo mtaa wa Livingstone na Aggrey mpaka mchikichi na mahiwa close huko utapata kwa bei nzuri na ukiuza utapata faida nzuri.
...
Vyombo vingine utavipata mtaa wa Aggrey na livingstone
.
Maua bandia utayapata mtaa wa Aggrey na sikukuu. Hapo kuna mchina yuko opposite na Bank ya NCBA.
.
Nguo za wanawake kama T_shirt skins, Bwanga, tops, gauni utapata mtaa wa Raha na Muhonda zaidi ingawa maduka ya nguo za wanawake yameganyika mitaa mbalimbali sana.
.
Vijora, Mitandio, Abaya na baibui utavipata mtaa wa nyamwezi na Narung'ombe jengo la Barcelona floor ya pili.
.
Nguo za wanaume kama suit, jeans, Track, shati, T_shirt, kadeti nk utavipata jengo la Mchikichi complex.
.
Shati quality za kiume chimbo ni kwa @welldone_turkish_fashions congo na narung'ombe
.
Pochi kariakoo makutano ya likoma na muhonda
.
Vifungashio kama makopo, chupa, mifuko, mabox ya bidhaa aina zote utapata mtaa wa Tandamti na sikukuu
.
Mnaulizia sana mtumba Grade A kuna marafiki zangu wanaleta mtumba mzuri ambao huwezi kujutia wako ilala Boma
.
Wale wa mtaji mdogo nenda ilala boma saa 11 asubuhi utapata mtumba ata nguo za 1000 ukauze minadani
.
Viatu vya kike vipo mtaa wa congo na narung'ombe, ukienda saa 11 asubuhi utajua machimbo ya wachina maana wengi wanashusha kutoka stoo asubuhi.
.
Viatu Vya kiume vipo Nyamwezi na Narung'ombe. Lakini ukihitaji viatu vya Mtumba hivyo utavipata mtaa wa Karume, nenda pia asubuhi saa 11.
.
Unahitaji Nywele, unahitaji rasta nenda mtaa wa jangwani na mafia. Huko kuna maduka mengi na mawakala wa viwanda vya rasta. Ni ule mtaa zinapopaki Daladala za makumbusho gerezani.
.
Kwa upande wa Vipodozi aina zote pia nenda huu mtaa wa Mafia na Jangwani hapo kuna duka maarufu la @kariakoovipodozi utapata vipodozi.
.
Lakini tusikalili kuna Machimbo mengine hayapo kariakoo ila wanashusha mizigo kwa bei ya chini na kuweka stoo.
.
Turudi kariakoo, mtaa huu wa mchikichi na nyamwezi kuna duka kubwa la vifaa na nguo za watoto wachanga, yaani nguo, mabeseni, matoroli, babyshioo, pot aina zote nk. Hilo jimbo kama una duka la watoto na wajawazito utanishukuru.
.
Mashuka ya uganda nenda kwa mchina opposite na Bank ya Crdb
.
Nguo za ndani Nenda makutano ya mtaa wa mchikichi na sikukuu. Hapo kuna duka kubwa mno utapata nguo za ndani jumla kwa aina zote.
.
Kuna Chimbo Waturuki wana vyombo imara vizuri vya kituruki pia wanakopesha kwa wenye maduka. Ni vizuri hata kwa matumizi binafsi
Chimbo gani lingine unaongeza lipi unatafuta? Endelea kwenye comments
.
Unataka number zao? Sijui kama hapa inaruhusiwa ila instagram kwenye page yangu ya @kelvinkibenje utapata machimbo yote na Number zao na updates.