Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Chimbo la sabuni zile za kunukia (za kuogea) hapo k/koo,msaada jamani nimeona fursa huku chalinze
 
Mambo Charty,
 
Charity naomba unisaidie namba yako ya simu, ni kwaajili ya kuomba mwongozo tu pls. Naona PM ipo secured.

Stay blessed.
sawa vingine ukitaka unasema tu nakuelekeza! ninavyovijua pia nitakua nakuongezea machimbo mapya maana supplier wengine wanafilisikaga hahaaahaa
 
Kituo cha msimbazi pale yanapopaki magari ya mabibo ndio chimbo la sabuni,mafuta ya aina zote,pafyumu na makolokolo kibao ya urembo yanapatikana mitaa ile
Yeees nimeshalipata mkuu dah utajiri si huu jamani!!!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
2017 huyu mchina atakuwepo bado Kiukweli nilipatafuta sikupaona kabisa
 
Naomba namba na Mimi nipajue
 
Wapo sana tena wamekua wengi cha msingi,uwe unadamka mapema ikiwezekana kabsa saa 1 asubuhi ikukute mtaa wa Narung'ombe na Congo.Wafanyabiashara wenzako wanapokua wanakusanya oda ya kuchangia box nawe uwepo ili upate kwa bei nafuu.Inakua kama mnada fulani hivi sample zinazungushwa.Ila angalia usitapeliwa usitoe pesa ako hadi uone mzigo sawa.
Huu uzi umesonga sana kitambo sana sijapita humu.Kila la kheri.
2017 huyu mchina atakuwepo bado Kiukweli nilipatafuta sikupaona kabisa
 
Nataka wanapouza cheni na urembo wa kike please nisaidie
 
Mkuu nielekeze na Mimi
Ukifika pale msimbazi kituo cha polisi si kuna kituo cha mwendokasi,ukiwa kama unaelekea fire mwisho wa kile kituo cha mwendokasi kuna barabara inaelekea kushoto kwenye maduka ya jumla ya rasta, nenda na hiyo barabara ikiwezekana ulizia kwa watu yalipo maduka ya rasta,ukifika kwenye hayo maduka ya rasta...maeneo hayohayo we ulizia duka la vipodozi kwa bei ya jumla,watu watakuelekeza maana ni chimbo haswaaa huwezi kupajua kirahisi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…