Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Hivi kumbe watu kama hawa bado wapo, ubarikiwe sana mkuu.
 
Du! Kwa jinsi unavyoelekeza ata MTU awemgeni awezi pote, balikikiwa sana.
 
Hata mtaji sina nakula kwa mama nalala kwa bibi
Ndugu usiongee kinyongo hivyo una mkufuru Mungu pambana..mtaji wa kwanza ni wazo sio pesa kuwa na mawazo ya kibiashara pesa itakuja kuwa kama nyenzo.. Nakupa akili moja huna mtaji wa hela..fanya hivi nenda kariakoo nenda kwa wale wamiliki wa maduka kama ya nguo au ya simu waombe uwe una piga picha bidhaa zao na kuzirusha kwenye mitandao wakupe bei za bidhaa zao na wewe jazia hela kidogo hata kama ukijazia 2000/= kwa kila nguo sio mbaya baada ya hapo anza kurusha kwenye social media ulizomo... Note uaminifu ni jambo la msingi na iwe silaha kwako daima.. Kama ni njema fanya kama sio njema washirikishe unao wajua hili wazo yote kwa yote woga wako ndio umaskini wako..kila rakheli
 
Wakuu nauliza kwakariakoo niwap naweza pata baloo la lady's koti zalezer
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa.Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale la si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Asante umenisaidia mnoo ila cna cha kukulipa
 
Habari. Napenda kujua sehemu ambayo nawezakupata vitu kama flash disc, memory card, earphone, head phones, betri za smu, redio ndogo za kuchaji, na taa na tochi za solar pamoja body spray hasa kwa kariakoo
Wakikujibu nitag mkuu
 
Hahhahah sasa wewe mie mkali wa hizi kazi tokea nipo chuo kitamboo nimeivuruga sana hiyo k.koo hahah hadi leo nipo yaani na sibanduki ng'ooo inabidi tuwasaidie wenzetu bana maana haya maisha mtu akikuongezea jero kwenye product ni kubwa sanaaaa. Na hivi vyuma vimekaza acha tu na wenyewe wale.Ila si unajua mjini wasioujua bado wengi utawapata tu maana hawapo humu JF .

Ngoja niwape chimbo la pochi za bei rahisi zile ronya na za kati 6000,8000,12000 lipo maeneo ya nyamwezi karibu na soko la shimoni kale kamtaa cha kati uje utokee msimbazi kota,karibu wanapouza maturubali, lingine lipo mtaa wa congo na aggrey kwa juu ghorofani kama unataka kutoka congo kituo cha basi pale wanauza high quality PU zao 22k,25k,28k,30 nk ambazo ukikuta kwenye botique ni mwendo wa 50k,70k hadi 100k. Pia tena hiyohiyo Congo/mchikichi pale katikati kwa ghorofani wanauza pochi eh bei chee tatizo lenu mnapita juu juu tu ingieni maduka ya ndani na chini yana mambo mazuri Wallet nazo mchikichi zipo za kumwaga za kiume na za kike bei chee hakikisha unaingia ndani kabisa kwenye vichochoro. Haya kwa wale wa mabegi ya kusafiria kuna mchina anazalisha mwenyewe maeneo ya Veta karibu na sofia house kule anakutengeneezea design unayotaka eh,pesa yako tu. Kuna kingine nimesahau? Danhappy
Mkuu wapi naweza pata machimbo ya jeans na t shirt nzuri
 
Back
Top Bottom