Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Watanzania tungekuwa na roho na wepesi kama wewe tungekuwa mbali sana. Hongera mkuu
 
Mi kuna machinga nilikuwa nachukua mzigo kwake,hivyo nampa pesa ye anazunguka kwenda kuchukua mzigo.Ukimuuliza asemi,siku nilienda na vijana wangu watatu ambapo yeye hakuwaona.Hivyo nilivyomkabidhi pesa akaondoka,vijana wangu wakamfuatilia mpaka wakajua maduka yote aliyoingia.Tangia siku hiyo hajaniona na majamaa wa madukani washanizoea hats bila pesa wananipa mzigo au wanatuma mkoani.
Kweli we ni rice cooker
 
Wakuu, wazo langu ni kwamba wanaoenda nje kununua bidhaa mbalimbali wangekuwa wanapeleka na kuuza bidhaa za Tanzania zenye uhitaji mkubwa huko ili Ku make super profit na kupunguza gharama za usafiri na accommodation mfano mzuri wa bidhaa hiyo ni madini (hasa dhahabu) wahindi wengi wanachukua kwa wingi na kwenda kuuza nje..je sisi hatuwezi?
Najua wazo langu sio jipya sana ila tatizo ni network na network yenyewe ipo humu
 
Kwa aliyepo Mbeya tafadhari naomba msaada wa kujua bei za mebaro ya viatu.
 
Jamani mabaro ya viatu vya mtumba naweza kupata wapi mazuri na kwa bei nafuu kwa DSM?
 
Ngoja nikupe machimbo eh best kizuri kula na mwenzio...Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule mnazi mmoja wengi wanaouza k.koo wanaenda kufata huko, Viatu navyo vinapatikana huu mtaa wa Narung'ombe na congo pale nenda straight kwenye maduka ya wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini nop unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile visandles wanauza 2500/pc. Cheni zama mchikichi katikati kuna mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki.Magauni nayo ingia ndanindani kule congo na aggrey wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka kutype ah.
Mimi sio mzoefu wa biashara hii , unaposema wanauza 4000 pc unamaanisha nini?
 
Anayejua kilipo kiwanda cha plastic kinachouza bidhaa bei nzuri anijuze
 
Kadi za Harusi na sherehe mbalimbali dizaini tofauti tofauti wapi naweza pata Kwa bei iliyopoa
 
Naombeni kujua wapi naweza pata mobile phone accessories kwa bei ya jumla yani, chargers, usb cables, head phones, chaji za simu za gari, memory cards, flash disks na computer accessories kwa bei nzuri na viwe durable
 
  • Thanks
Reactions: Fdt
Back
Top Bottom