Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Tanzania nchi ya ajabu sana,miwani za Tiba wanauza waha kwa jumla ambapo hata shule hawakwenda.Wakati wenye profession wamelala kwenye ajira,unakuta jamaa anakupa mzigo hata kuandika jina kwenye risiti anambwela.Bongo wasomi wakishtuka biashara itanoga
Miwani za wapi wanauza Jumla, tuelekeze kamanda
 
Mfano kuna chimbo moja wanauza viatu vya kiume mfano Sebago pale wanauza Tsh 40,000 wakati huo ukipiga hatua mbili upande mwingine same sebago inauzwa 60 na maeneo ya pembezoni ni hadi 100K.
Litaje ilo Chimbo basi
 
Jamani machimbo ya vifaa vya pikipiki na being nafuu, kwa kariakoo sehemu gani yanapatikana wapi?
Kuna bingwa mmoja, maarufu Saidi, anauza spea zote za pikipiki, karibu na shule ya Uhuru na msimbazi,

Ukiingia duka lolote la spea za pikipiki, muulize duka la Saidi liko wapi, Saidi mapikipiki
 
Nani ANALIJUA DUKA (CHIMBO) LA VITAMBAA VYA SUTI. Naomba atuambie
 
Msaada tafadhali mwenye ako anajua wapi kuko na chimbo la suruali kali za kadeti, vitambaa na suti kwa kariakoo!!
 
Naomba niunge mkuu
Jamani eeh mwenye group kagoma anasema wanajf wengi hawaaaminiki kakataa katu katu so msije hata pm kutaka kuungwa. This chapter is closed poleni sana ila pia mnaweza kutafuta fursa kwingine.
 
Angalia wanaokupa namba wasipokudalalia watasepa na mtaji vyuma vimekaza
 
Kwa ujumla wafanya biashara wa Dar ni waaminifu sana na niwakalimu kuliko sisi wa mikoani maana ukituma pesa ikatokea mzigo uloagiza pesa imebaki utashangaa unapigiwa sm nakuambiwa pesa imebaki kias flani uamuz unabaki kwako uludishiwe au uongeze mzigo ,mm hii imetokea Mara kibao laki wauzaji wa jumla uku mikoan usishangae anakuibia ukiwa dukani kwake,Ongela zenu wauzaji wa jumla was Dar.
Yaaah hasa utaratibu wao unaweza waachia list ya bidhaa unazotakaa ukaendelea na mishe zako ukirudi unakuta wameshapack na hawapunguzi hata bolt, njoo ss huko nanjilinji bila kusimamia utajuta. Kwa uaminifu tu kwenye mizigo ya wateja kkoo wapo juu.
 
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
Visandles vya 2500 pic vinakua vingap mkuu xamahn lakn
 
Back
Top Bottom