Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

Wafanyabiashara wa mikoani mnaochukua vitu Kariakoo, njooni tujuzane machimbo ya bidhaa

WAPI NITAPATA CHIMBO LA VITU HIVI VIFUATAVYO
-Earphone za bei chee
-Charger
-usb za urefu mpk mita tano imara za bei chee
Vinote book na daftar pen kwa bei jumlaa
Kalamu kwa bei jumlaa

Nitashukuru sana
Earphone, USB na cherger nenda K.koo mtaa wa Aggrey /Likoma Street
Peni, notebook, daftari nenda Uhuru/Congo street
 
God bless u
Ngoja nikupe machimbo best. Kizuri kula na mwenzio. Vitenge mara nyingi machimbo yake yapo NIDA kule Mnazi Mmoja wengi wanaouza Kariakoo wanaenda kufuata huko. Viatu navyo vinapatikana huu Mtaa wa Narung'ombe na Congo pale nenda straight kwenye maduka ya Wachina yaani sio wale machinga wanaomwaga chini, nop. Unazama dukani utakuta zile simple wanauza 4000/pc na vile vi-sandles wanauza 2500/pc. Cheni zama Mchikichi katikati kuna Mchina anauza mpaka 2000-3000/dz na hazipauki. Magauni nayo ingia ndanindani kule Congo na Aggrey, wanauza nayo bei chee 6000-8000-1000-16000/pc. Vingine siku ingine nitakwambia nimechoka ku-type ah!
 
Wakuu salama poleni na majukumu.

Nilikuwa naomba kupata msaada wenu, mimi natamani kufanya biashara ya vitenge ila sifahamu mzigo unaupata vipi Kariakoo.

Anayefahamu chimbo bei ya jumla tusaidiane.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wengine ndo tunagutuka kumbe kushakucha
Mi ninachokifanya naenda nai nafunga Mzigo wangu nikifika dukani nauza jumla na reja reja bei sawa na dar nahakikisha kila pc1 inatoa efu 4 na nasafari kila wiki kwa sehemu niliyopo nategemewa na wenye maduka na wanaouza kwa kutembeza muhimu fanya utafiti wa eneo ulilopo na kujua aina ya nguo zenye mzunguko mkubwa maana biashara si kupamba duka bali bidhaa zitoke.

K/koo siku izi wanamix copy na og na wanakuuzia bei moja.. @honort hope nimekupa idea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom