The Happiness
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 6,989
- 45,411
Nilipita duka moja anauza chupa 3-4 kwa 20,000, sasa sjajua kama bei yake itakuwa ni jumla kwako!Ni wapi kariakoo naweza pata chupa hizi na bei yake kwa jumla
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nilipita duka moja anauza chupa 3-4 kwa 20,000, sasa sjajua kama bei yake itakuwa ni jumla kwako!Ni wapi kariakoo naweza pata chupa hizi na bei yake kwa jumla
Hilo ni jambo hatari mnoNamaanisha kununua kwenye mtandao wa Alibaba na SIO KWENDA CHINA physically.. Alibaba haiitaji mkubwa unaweza kupata supplier akakufungia mzigo hata wa laki moja au hata chini ya hapo inategemeana na bidhaa.Cha msingi ujifunze namna ya kuutumia Kwa kusearch bidhaa, kuwasiliana na supplier, kulipia na kusafirisha..
Hatari yake Iko wapi? Mimi kila siku nanunua huko na kusafirisha na silent ocean etc ...Hilo ni jambo hatari mno
Mzigo unachukua siku ngapi kufika?Hatari yake Iko wapi? Mimi kila siku nanunua huko na kusafirisha na silent ocean etc ...
Mwezi mmoja unachukua unakuwa umefika .Mzigo unachukua siku ngapi kufika?
Shida ni hivi ni ngumu nichukue milion 20 niagize mzigo kwa njia hiyo ya onlineMwezi mmoja unachukua unakuwa umefika .
Kwa mill 20 nakushauri nenda china physically...Shida ni hivi ni ngumu nichukue milion 20 niagize mzigo kwa njia hiyo ya online
njoo dm.Msaada wa dharura tafadhali natafuta chimbo au mtu anayejua mahali naweza pata spea za pikipiki aina zote kwa bei ya wholesale tafadhali
Nitafutie na Mie nataka nianze biashara ya kuuza jersey ni join kw magroup ya jersey na beizake 0754984454Ni add na mm bosi
Mkuu nahitaji tufanye biasharaZilishaisha boss,
Labda Kama Unahitaji nikupakilizie mzigo
Mkuu habari naweza kuja pm?Habari Wadau Nashukuru Nimerudi mkoan salama Jana Mrejesho kwenye ununuzi wa bidhaa za yebo yebo Na slippers Zipo Mtaa wa Msinbazi kariakoo kuna Ndala, slippers,yebo yebo Za Kila Aina Bei za jumla nilizokutana nazo zipo za 2600,2800,3500,5500,6000 kuanzia pic's 6 Nami nimeondoka Na mzigo wa Kuanzia biashara pic's 107 nizizuungushe masokoni nteleta mrejesho Wakuu.
Nataka chimbo za zile tshirt na bukta feki, zinakua na picha picha za watu maarufuNaona uzi umepoa. Ngoja nishushe vitu.
.
Unataka Kufanya Biashara ya Vyombo vya plastiki kama viti, meza, vikombe, majagi, mabeseni nk. maduka ya viwanda yapo kariakoo mtaa wa Livingstone na Aggrey mpaka mchikichi na mahiwa close huko utapata kwa bei nzuri na ukiuza utapata faida nzuri.
...
Vyombo vingine utavipata mtaa wa Aggrey na livingstone
.
Maua bandia utayapata mtaa wa Aggrey na sikukuu. Hapo kuna mchina yuko opposite na Bank ya NCBA.
.
Nguo za wanawake kama T_shirt skins, Bwanga, tops, gauni utapata mtaa wa Raha na Muhonda zaidi ingawa maduka ya nguo za wanawake yameganyika mitaa mbalimbali sana.
.
Vijora, Mitandio, Abaya na baibui utavipata mtaa wa nyamwezi na Narung'ombe jengo la Barcelona floor ya pili.
.
Nguo za wanaume kama suit, jeans, Track, shati, T_shirt, kadeti nk utavipata jengo la Mchikichi complex.
.
Shati quality za kiume chimbo ni kwa @welldone_turkish_fashions congo na narung'ombe
.
Pochi kariakoo makutano ya likoma na muhonda
.
Vifungashio kama makopo, chupa, mifuko, mabox ya bidhaa aina zote utapata mtaa wa Tandamti na sikukuu
.
Mnaulizia sana mtumba Grade A kuna marafiki zangu wanaleta mtumba mzuri ambao huwezi kujutia wako ilala Boma
.
Wale wa mtaji mdogo nenda ilala boma saa 11 asubuhi utapata mtumba ata nguo za 1000 ukauze minadani
.
Viatu vya kike vipo mtaa wa congo na narung'ombe, ukienda saa 11 asubuhi utajua machimbo ya wachina maana wengi wanashusha kutoka stoo asubuhi.
.
Viatu Vya kiume vipo Nyamwezi na Narung'ombe. Lakini ukihitaji viatu vya Mtumba hivyo utavipata mtaa wa Karume, nenda pia asubuhi saa 11.
.
Unahitaji Nywele, unahitaji rasta nenda mtaa wa jangwani na mafia. Huko kuna maduka mengi na mawakala wa viwanda vya rasta. Ni ule mtaa zinapopaki Daladala za makumbusho gerezani.
.
Kwa upande wa Vipodozi aina zote pia nenda huu mtaa wa Mafia na Jangwani hapo kuna duka maarufu la @kariakoovipodozi utapata vipodozi.
.
Lakini tusikalili kuna Machimbo mengine hayapo kariakoo ila wanashusha mizigo kwa bei ya chini na kuweka stoo.
.
Turudi kariakoo, mtaa huu wa mchikichi na nyamwezi kuna duka kubwa la vifaa na nguo za watoto wachanga, yaani nguo, mabeseni, matoroli, babyshioo, pot aina zote nk. Hilo jimbo kama una duka la watoto na wajawazito utanishukuru.
.
Mashuka ya uganda nenda kwa mchina opposite na Bank ya Crdb
.
Nguo za ndani Nenda makutano ya mtaa wa mchikichi na sikukuu. Hapo kuna duka kubwa mno utapata nguo za ndani jumla kwa aina zote.
.
Kuna Chimbo Waturuki wana vyombo imara vizuri vya kituruki pia wanakopesha kwa wenye maduka. Ni vizuri hata kwa matumizi binafsi
Chimbo gani lingine unaongeza lipi unatafuta? Endelea kwenye comments
.
Unataka number zao? Sijui kama hapa inaruhusiwa ila instagram kwenye page yangu ya @kelvinkibenje utapata machimbo yote na Number zao na updates.
Karibu Sana bossMkuu habari naweza kuja pm?
Hii cabs instagram mbona hajapost bidhaa muda mrefu na haionyeshi kama anauza vijora vya paziaCabs