DOKEZO Wafanyabiashara wa ndizi mbivu Dar huchovya kwenye kemikali ili kuziivisha ndani ya muda mfupi. Afya za watu hatarini

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mimi ndiszi hizosizitaki sio sababu ya kuzivundika hapana sio tamu............ mmetoka wenye karanga mmehamia kwenye ndizi. Ndizi ni rahisi sana kuiva jamani hata zikisafirishwa mpk ufika huku zishaanza kuiva
Mkuu. ebu tujuze huko kwenye karanga kuna utalaamu gani
 
Maganda ya ndizi ya siku hizi huwa yanatoa harufu. Tunalishwa madawa kila sehemu nyanya, mboga za majani, kuku😭
 
Nguruwe kulishwa ARV pombe chafu nyingine mpka zinatengenezwa na maji ya betri, kuku kuchanganyiwa uzazi wa mpango kwenye lishe yao , umri wa kuishi ni miaka 40 ukiwa mwenye nguvu 50🤔
😔Aisee
 
Siku hizi kwa wakazi wa pwani na daresalam matunda mengi sio salama. Kiwangwa wanapulizia dawa kwenye mananasi yaive haraka. Unakuta nanasi nje limeiva ndani jeupe kama karatasi. Maembe pia hali kadhalika unakuta embe limeiva ukilila ni chachu kama bichi. Machhungwa n.k. Awamu hii hakuna ufatiliaji kwa iyo vitu feki ni vingi sana.
 
Mhhhh, kuna siku nilinunua yale maembe maboribo ya kukata, yameiva vizuri tu lkn yalikuwa machachu hatari hakuna aloyaweza kuyala. Siku hizi mambo ni mengi kwa kweli, zamani hatukuyaona haya, matunda mengine mengine yanaiva na mengine kufikia kuoza mtini.
 
Hizi ndizi sijui kwa nini mimi sina mzuka nazo kabisa. Kwanza ndizi kubwa kama dodoki, kwa sisi zanzibar tushazoea ndizi zetu za pukusa, sema ndio zinauzwa ghali.
nasikia baadhi wazanzibar wengi hawapendi kununua ndizi kutoka tanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…