KERO Wafanyabiashara wa Temeke Mwisho tumekaa kwenye eneo hili kwa miaka 15, leo tunaambiwa tuondoke kuna mgogoro

KERO Wafanyabiashara wa Temeke Mwisho tumekaa kwenye eneo hili kwa miaka 15, leo tunaambiwa tuondoke kuna mgogoro

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wafanyabiashara katika eneo la Temeke Mwisho tumepewa barua za kutakiwa kuondoka kupisha eneo hilo kwa ajili ya mwekezaji. Viongozi wanaeleza kuwa eneo hilo lina mgogoro, huku kukiwa na taarifa kuwa kampuni ya GSM ndiyo inayotarajiwa kuwekeza.

Hata hivyo, wafanyabiashara tulikabidhiwa eneo hilo kwa ajili ya shughuli za biashara zaidi ya miaka 15 iliyopita. Tumeshangazwa na hatua ya kuitwa wavamizi na kutakiwa kuondoka, licha ya kuwa tumekuwa tukilipa kodi na ushuru kwa kipindi chote hicho.

Wafanyabiashara tunaomba haki itendeke na mamlaka husika zishughulikie suala hilo kwa kuzingatia mazingira na haki zetu.
 
Back
Top Bottom