KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

KERO Wafanyabiashara ya chakula acheni kurudisha mabaki

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Utashangaa kwenye thread hii kuna mdau analalamika eti chakula tunachokula migahawani huwa hali kwa sababu ya uchafu cha kuchangaza huyohuyo analamba papuchi.
Sijui anakwepa kitu gani
😂😂😂😂
 
Elimu inahitajika sana kwa wafanyabiashara hususani wa chakula! Kuna tabia ya kulamba ulimi kupakaza mimate kwenye vidole kisha kufungua mfuko wa nylon na kukuwekea bidhaa kama nyanya ,bamia ,carrot ,hoho etc

Kuna tabia ya kupuliza mifuko ya nylon na kufunga karanga ,miwa ,ubuyu ,korosho etc ,elimu inahitajika sana ni chanzo cha magonjwa ya TB ,Hep B etc
Umenikumbusha kuna siku nilienda dukani kununua Skonzi, nimefika muuza duka katoka kupimia watu maziwa, alichofanya akapaka vidole mate ili afungue mfuko baada ya hapo akachukua mfuko wa Skonzi akatoa na mikono yake hiyohiyo yenye mate na maziwa.

Nilichukia sana, ila nikaamua kuondoka tu. Zile Skonzi zikaishia kwenye takataka na ndiyo ukawa mwanzo wa kununua Skonzi mfuko mzima ili kuepukana na hii adha maana kuna watu usafi ni 0.
 
Kuna hii tabia ya kurudisha mabaki ya mteja kwenye chakula Kwa wafanyabiashara hasa wa maeneo ya kawaida japo huwa hatuoni ila utakutana nayo tu.

Juzi Kuna mtu kasema aliwahi shuhudia mama ntilie anarudisha mchuzi uliobakishwa na mteja kwenye sufuria ya mboga nikakumbuka visa vyangu, silagi Kwa mama ntilie ila chips haziepukiki.

Pia soma: Huwa unakagua usafi sehemu unayoenda kupata chakula?

Eneo la kwanza ni Mikocheni karibu na hospital kubwa sana, wakati nakula chips mayai kufungua katikati nakuta nzi wamenasa ilibidi njikaze tu kuwaondoa nsije tupa chakula na nna njaa.

Eneo la pili Ubungo mitaa ya hosteli ndanindani kwenye hotel kama nyota tatu, nikiwa na rafiki ikaagizwa chips mayai na nyama, wakati nakula katikati nakuta mifupa midogomidogo ya kuku ilikwishaliwa liwa imenasia, na pieces za kabichi, means mteja akibakisha wao wanatoa kile kilichobaki wanarudisha kwenye kisafi wanachanganya.

Juzijuzi Tena Niko Magomeni, kwenye chips tu pembeni ya main Rosa, chips mayai nakula katikati nashangaa naona ugumu kufosi naibuka na toothpick kama tatu zimelala katikati ya mayai. nkitafuta nakuata vipande vya nyama.

Sijawahi kutana na haya mambo mtaani kwetu ila maeneo yenye biashara ndo nakutana nayo.

Mbona mnatufanyia hivi, imagine mtu unahangaika tangu asubuhi hata kunywa maji hukumbuki, unaamua kupoza tumbo unaletewa vyakula vilivyorudishiwa mabaki?

What if huyo aliekula hapo akabakisha ana maradhi yanayoambukizwa Kwa mate kama hepatitis?
What if akiwa anakula kapiga chafya vikarukia humo?
What if wamewekeana sumu au madawa?

Mteja anatoa pesa kamili Kwa kile anachostahili hata mkimwaga hayo mabaki shida yenu Iko wapi, si unauza kama ulivyoplan? Kwanini mnarisk Maisha ya wengine kutafuta extra profit toka kwenye kilekile mlichozalisha. Mnapata hasara mkimwaga ilhali kishalipiwa?
Mnaua biashara za wengine pia.

Badilikeni!!
Pale makumbusho kitimoto rosti, saa saba usiku, jamaa kapiga mifupa na nyanya, kaweka mezani kasepa,mifupa haina nyama, ila tulimsaka mpaka nyumbani kwake Tandale, akalipia usafiri na kila kitu
 
Pale makumbusho kitimoto rosti, saa saba usiku, jamaa kapiga mifupa na nyanya, kaweka mezani kasepa,migupa haina nyama, ila tulimsaka mpaka nyumbani kwake Tandale, akalipia usafiri na kila kitu
Rosti Hilo😂😂
 
Mi ndo maana huwa nikibakisha chakula nakinawia natupia stick na tissue nachanganya na chakula au km kuna upenyo natupia paka ama mbwa, nakifanya kisiuzike tena kwa namna yoyote
 
Mi ndo maana huwa nikibakisha chakula nakinawia natupia stick na tissue nachanganya na chakula au km kuna upenyo natupia paka ama mbwa, nakifanya kisiuzike tena kwa namna yoyote
Walivyopinda wengine .watachuja
 
Bila kusahau wengi wa wauza samaki wa kukaanga wa mtaani
Picha linaanza wengi hawakaangi hao samaki mazingira safi
Ukinunua anashika samaki kwa mikono yake ndiyo anakuwekea kwenye kifungashio
Mikono hiyo hiyo anajikuna, anashika hela na mikono hiyo hiyo anaitumia chooni
Yani ganzi sana aisee
 
Back
Top Bottom