Wafanyakazi Mastermind Tobacco walalamika kufanya kazi muda mrefu bila kupewa ajira rasmi

Wafanyakazi Mastermind Tobacco walalamika kufanya kazi muda mrefu bila kupewa ajira rasmi

NBica

Member
Joined
Sep 13, 2010
Posts
39
Reaction score
36
Kampuni ya Mastermind Tobacco Tanzania Limited inayopatikana Jijini Dar es Salaam maeneo ya Tazara imelalamikiwa na baadhi ya Wafanyakazi wake kwa kuwafanyisha kazi muda mrefu bila kuwapatia ajira.

Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi hao ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani Wafanyakazi hao ambao hawajaajiriwa wa kuanzia miaka saba, mitano na mingineyo iliyopita akieleza si utaratibu wa kazi.

Amesema kukosa kwao ajira kuna sababisha kupoteza stahiki zao kwa matukio kama ajali kazini, vifo na huduma nyingine za kijamii kama Mifuko ya Hifadhi za Jamii kama NSSF na nyinginezo.

Alisema pamoja na kampuni kuifanyia maboresho lakini bado maisha ya wafanyakazi hao wenye idadi kati ya 50-60, maisha yao yanazidi kuwa magumu.

Aidha Mfanyakazi huyo amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuwasaidia Wafanyakazi hao kwenye suala lao.

Mfanyakazi huyo alisema mojawapo ya wafanyakazi wanaolalamika kukosa ajira ni wa kitengo cha mauzo.

Ofisa Rasilimali watu wa kampuni hiyo, Erick Steven hakuna tatizo lolote baina ya pande mbili kwani kila kampuni inataratibu zake za ajira.

Steven amesema wanafahamu taratibu za kazi na hawawezi kutoa ajira bila mpangilio, hivyo kila jambo na wakati wake.
 
Back
Top Bottom