Jana nilisema nitatoa takwimu na mahesabu jinsi working culture ya Tanzania inavyoendekeza uvivu na umasikini.
Kwanza tuanze kwa kuweka the present Tanzanian working situation:
- Mfanayakazi anafanya kazi nchini kwa masaa 8 kwa siku
- kwa wiki kazi ni siku 5(jumatatu hadi ijumaa)
- Hivyo kwa wiki mfanyakazi atafanya kazi masaa 40
- Mwaka una siku 365, ondoa siku 30 za likizo, na siku 15 pengine mtu anaumwa au sikukuu, kwa hiyo mtu anafanya kazi kwa mwaka siku 330.
- Katika mwaka huo mfanyakazi wetu mpendwa ana faya kazi kwa masaa 330*8=2,640 hrs.
Nimefanya kazi na kampuni moja ya kigeni, kutoka nchi ya dunia ya kwanza, wao working culture iko hivi:
- Mfanyakazi ana fanya kazi kwa masaa 11 kwa siku(kuanzia 12.30 asubuhi hadi 12.30 jioni, mapumziko ya saa moja mchana)
- kwa wiki kazi ni siku sita, jumatatu hadi jumamosi hivyo kwa wiki masaa ya kazi ni 66!
- Katika mwaka huo huo wa mtanzania pamoja na siku 45 za likizo na sikukuu, wenzet wanapiga kazi 330*11=3630 hrs!!!
Sisi katika mtaji ule ule wa MUDA tulionao wenzetu mfanyakazi anafanya kazi masaa 3, 630 kwa mwaka , wakati sisi mfanya kazi mtanzania( tena mwaminifu) anafanya kazi kwa masaa 2,640 tu.
Yaani wenzetu mfanyakazi anafanya kazi kwa ziada ya masaa 1,010 hrs kwa mwaka, kuliko mfanya kazi wetu!!!
Kwa scenario hiyo kwa nini wenzetu wasiendelee kwa kasi wakati sisi hapa tunavulimilia mediocre working tendencies?
Mkuu tafuta msaada.
Una tatizo la wale masikini walioridhka na kila wakiona mfanyabiashara anainukia ,yeye anaona anaibiwa.
Jitoe katika huo unyonge wa kujitakia.