DPW wakiwasili kwenye bandari zetu mengi yatabadilika for good or for worse. Japo ningependa uwazi zaidi juu ya mkataba na DPW, najua kuna mambo yatabadilika na kuwa mazuri na mengine yatakuwa sio.
Je ilishindikana kabisa kwa Serikali kuweka nguvu zake na kuibadilisha bandari ya Dar kuwa kama tunavyotaka DPW wafanye? Kama ni kweli tumeshindwa, basi tuna safari ndefu ya kujenga nchi yetu na kuleta maendeleo yetu. Kwa hakika tunaweza kusema sasa kuwa mchawi wa maendeleo ya mtanzania sio mwingine ni mtanzania mwenyewe.
Nafikiri watu hawasemi tu ila naamini tungekuwa na ujasiri wa kutosha tungemwita mkoloni aliyetoka aje tena atuongoze hadi pale tutakapokuwa tayari kujitawala. Je tunaweza kujitawala? Ndiooo lakini hili ni jibu la kisiasa tu, hata sisi wenyewe tunajua wazi kuwa hatuwezi. Ndio maana tunawaita wakoloni watusaidie japo kipande kwa kipande.
Wafanyakazi wa bandari mliozoea kupiga mkiwa maofisini mjiandae kisaikolojia kwani sasa mtakuwa chini ya management nyingine. Licha ya matumizi makubwa ya TEHAMA kwenye kila hatua za kazi yenu, ile milango ya nyuma utafungwa na madili yatakuwa magumu sana. Wengi wenu hamna viwango na mtafyekwa kwelikweli. Wavivu, wazembe, na wezi mjiandae. Je hii ni faida mojawapo ya kubinafsisha lango letu kuu? Pengine.