Wafanyakazi bandari fungueni masikio na akili zenu kuhusu hawa jamaa wa DP World endapo watashika madaraka. Kwenye kikao cha Prof Mbarawa na wahariri wa magazeti nilimsikia katika mkuu wa wizara ya viwanda na biashara akisema hakuna mfanyakazi atakaepunguza na hawa jamaa wa DP World. Hawa jamaa mfumo wao wa utendaji wa kazi uko DIGITILIZED. , Huenda kazi inayofanywa na watu 100 bandarini kwa sasa itakuja kufanywa na watu 10 .Sijui kama management ya hawa jamaa watakubali kuwa na wafanyakazi wanaokuja kuja kazini kucheza bao na kuwalipa mshahara kila mwezi. DP World sio wajomba zetu , kwenye utendaji wao wataangalia faidi , kuwa na wafanyakazi mzigo sio mpango wao ndio maana mnapiga kelele bandari haileti faida kumbe kuna wafanyakazi wengi ni mzigo na wengine ni hewa