Wafanyakazi wa TRA nanyi fungueni maduka Kariakoo mlipe kodi hizi

Wafanyakazi wa TRA nanyi fungueni maduka Kariakoo mlipe kodi hizi

Mkunazi Huna hata kibanda cha biashara unaongea nini ! Wewe kaa kimya subiria mshahara tena upo ofisini hufanyi kazi zaidi ya kuleta uchochezi kwenye mitandao
 
Anamaanisha kuwa utitiri wa kodi umekuwa mkubwa sana, pamoja na kodi zote hizo bado running costs za ofisi zipo pale pale. Mkuu kama umewahi kumiliki walau duka utaelewa wanachoongea.
Wafanyabiashara wanatamani kusiwe na kodi yoyote......

Hata wafanyakazi pia....ila wao hubanwa kupitia MISHAHARA yao......
 
Watu hawakatai kulipa kodi bro issue ni iwe kodi rafiki na wao wapate kuishi ni dhahiri hujapitia kitengo hicho cha biashara,
Ikiwa mfanyabiashara analalamikia Kodi.....vipi mfanyakazi wa umma na mwisho kabisa vipi mlaji wa mwisho ambaye ndiye abebaye mzigo mzito?!!!!
 
Acha kumuona The Boss hajui jambo lipeni kodi kwa manufaa ya nchi yenu.

Store kuna walakini wa bidhaa watu wanauza mizigo juu kwa juu , watu hawataki kufata sheria za kodi risiti hamtoi na bado mnaona mnaonewa na mamlaka iliyofata tu miongozo ya iliyopewa na bunge.
Hawataki kulipa kodi....ndiyo silka ya mfanyabiashara.....ndiyo silka ya mfanyakazi(yeye hubanwa tu).....dunia haijaumbwa jana....[emoji1787][emoji1787]
 
Sirdirashy!
Ni bora na wewe kuwa mwelewa wa mambo kuliko kukurupuka! Mambo ya Kkoo tuachie sisi wachakataji wa financial information! Wewe nakuomba uendelee na hayo yako unayoyafanya limbukeni wewe!
Lipeni kodi hivi unaona nchi zilizoendelea zimeendelea kwa ajili ya nini kama sio kodi China tu hapo fine ya kukwepa kodi ni $250,000. Na hizi ngojera zote kodi watu inawauma nakutaka kuikwepa ndomana wanatoa hizo rushwa kwa maafisa sasa kama kuna mzalendo ataje majina aliempa hizo rushwa wakamatwe wote wapelekwe korokoroni[emoji23][emoji23] alietoa na aliepokea.
 
Mkunazi Huna hata kibanda cha biashara unaongea nini ! Wewe kaa kimya subiria mshahara tena upo ofisini hufanyi kazi zaidi ya kuleta uchochezi kwenye mitandao
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Niko ofisini hapa kazi zimepungua natambaa tu JF....sikiliza mgosi nimezaliwa familia ya biashara.....nina kaduka anakasimamia mdogo wangu.....

Acheni visingizio lipeni kodi.....binafsi ninakatwa tena kubwa tu ... kabla mshahara haujaingia katika akaunti yangu......shubamit!!!
 
Unapo lipa kodi unatakiwa kila matumizi unayofanya uyaorodheshe kwenye huduma kisha unatowa kwenye kodi knachobaki ndio unalipa. Mbona wahindi hawalalamiki?

Tatizo kubwa tunalo ni kwamba hatuna elimu ya namna ya kulipia kodi, ndio maana tunasema sema ovyo kulalama. Mfano, bidhaa umenunua milioni 500. Si unarisiti ya kununulia? Umelipa gharama za usafiri kupeleka saiti, si unapata risiti? Uchukuzi na kodi ya jengo la ghala, risiti si unayo? Malipo ya umeme na fire extinguisher, si unazo risiti? Gharama za ulinzi na insurance ya mali ghalani, si unayo risiti? Matumizi ya mafuta ya gari kwa mwezi kuenda kazini, si unazo risiti? Chakula na vinywaji kwa wakati wa kazi, si unazo risiti? Bima ya gari, bima ya afya ya watoto, na bima ya duka lako, si unazo risiti?

Ukishakusanya zote hizo, unatowa na kiwango cha kodi uliyolipa wakati wa kununua bidhaa toka kwenye ile uliyouza wewe. Kilichobaki ndo unalipa TRA. Wenzenu wahindi wanaweka kumbukumbu zote, ndo maana hata mchicha wananunua supermarket ili wabaki na risiti ili wakadai tax return wakati wakulipa kodi yako binafsi.

Tunakwama wapi waungwana?
 
Japo wafanyabiashara wanachangamoto nyingi dhidi ya TRA lakini pia wapo wafanyabiashara wengi walaghai. Naona sana kwenye biashara zao hawatoi risiti na hata kama akitoa risiti basi kaiandikia pesa ya chini sana. Hv mtu ananunua mzigo wa milioni anaandikiwa risiti ya laki moja
Wasipofanya hivi kwa mlolongo wa kodi wanaowekewa nadhani mwaka kesho hutawakuta hapo walipo ni either watakuwa wamegeukia kupiga winga au wameenda kulima.

Ukisema mtu afanye biashara kiuaminifu 100% hakuna atakaetoboa biashara bongo ni pasua kichwa.
 
Unapo lipa kodi unatakiwa kila matumizi unayofanya uyaorodheshe kwenye huduma kisha unatowa kwenye kodi knachobaki ndio unalipa. Mbona wahindi hawalalamiki?

Tatizo kubwa tunalo ni kwamba hatuna elimu ya namna ya kulipia kodi, ndio maana tunasema sema ovyo kulalama. Mfano, bidhaa umenunua milioni 500. Si unarisiti ya kununulia? Umelipa gharama za usafiri kupeleka saiti, si unapata risiti? Uchukuzi na kodi ya jengo la ghala, risiti si unayo? Malipo ya umeme na fire extinguisher, si unazo risiti? Gharama za ulinzi na insurance ya mali ghalani, si unayo risiti? Matumizi ya mafuta ya gari kwa mwezi kuenda kazini, si unazo risiti? Chakula na vinywaji kwa wakati wa kazi, si unazo risiti? Bima ya gari, bima ya afya ya watoto, na bima ya duka lako, si unazo risiti?

Ukishakusanya zote hizo, unatowa na kiwango cha kodi uliyolipa wakati wa kununua bidhaa toka kwenye ile uliyouza wewe. Kilichobaki ndo unalipa TRA. Wenzenu wahindi wanaweka kumbukumbu zote, ndo maana hata mchicha wananunua supermarket ili wabaki na risiti ili wakadai tax return wakati wakulipa kodi yako binafsi.

Tunakwama wapi waungwana?
[emoji2956]

Mswahili na kulipa KODI ni sawa na MATE YA MBWA kwa mswalihina......[emoji1787]
 
Tra anahusikaje na Bima ya afya?
Umeme?
Ulinzi?
Mishahara ya wafanyakazi wako?

Ada za watoto wako??

Hivi vyote ndo visingizio msilipe kodi???

Lipeni Kodi ....
Wenye akili wameelewa ila kilaza kama wewe hauwezi elewa alichoamanisha
 
Wasipofanya hivi kwa mlolongo wa kodi wanaowekewa nadhani mwaka kesho hutawakuta hapo walipo ni either watakuwa wamegeukia kupiga winga au wameenda kulima.

Ukisema mtu afanye biashara kiuaminifu 100% hakuna atakaetoboa biashara bongo ni pasua kichwa.
Kwanini hapa nyumbani biashara iwe pasua kichwa ?!!!

Duniani sisi ndio wa kwanza kufanya biashara ?!!!!

Mtanzania....hususani MSWAHILI....hataki/haweki kumbukumbu ya RISITI ZA MLOLONGO WA BIASHARA YAKE....anachojua ni kuangalia na kutaka FAIDA ya haraka na KUBWA TU....Kodi ni sawa na ZAKA misikitini na makanisani.....zaka ni hiyari ?!!! Zaka hutolewa kutokana na kujisikia/kuwiwa kwa muumini?!!!![emoji15][emoji1787][emoji1787]
 
Tra anahusikaje na Bima ya afya?
Umeme?
Ulinzi?
Mishahara ya wafanyakazi wako?

Ada za watoto wako??

Hivi vyote ndo visingizio msilipe kodi???

Lipeni Kodi ....
Kichwa box kauli za waenda kuzimu hizi
 
Tatizo la wafanyabiashara ni ukweli, wafanya wengi wa bongo ukweli kwao ni sumu. Siyo kwa wateja wao tu hata jinsi ya kulipa kodi ni udaganyifu kwenda mbele. Kodi ni sheria, na pia kodi ni maelewano. TRA wanacheza muziki unaopigwa na wafanyabiashara. Ukisema uongo kwenye biashara zako wakati ukweli unaonekana lazima wakubane tu. Wangekuwa waaminifu na kutoa risiti kwa kadri anavyouza hili suala la store na mengine yasingekuwepo, kumbuka TRA wanajua mbinu nyingi sana wanazotumia wafanyabiashara kukwepa kodi. Mzigo unaingia usiku bandari bubu, TRA watajuaje? Inabidi waje store. Nchi nyingi tajiri zimewekeza kwenye TRUST, ukiweka au kufanya UONGO wewe unashtakiwa na kufungwa na faini juu. Tatizo la baadhi watendaji wengi wa serikali ukishikwa unakwepa kodi wao wanaomba Rushwa, kwa mchezo huu ni sawa Paka na panya.

Kukomesha hili tatizo ni serikali kuweka mazingira mazuri ya kazi na mishahara inayoendana na hali halisi.
Kuwachukulia hatua kali wakwepa kodi na wala rushwa.
 
Ikiwa mfanyabiashara analalamikia Kodi.....vipi mfanyakazi wa umma na mwisho kabisa vipi mlaji wa mwisho ambaye ndiye abebaye mzigo mzito?!!!!
Tofautisha mtu aliyesajiliwa VAT na ambaye hajasajiliwa VAT , aliyesajiliwa VAT ni rahisi ile 18% kuicharge kwa mlaji wa mwisho

Ila huku mtaani ni tofauti mkuu , Yani unachosoma shule na unachofanya kazi ni different. Ukiuza kwa kuchaji final user 18% mwenzio hachaji hicho utamuuzia nani?

Si vizuri watu kukwepa kodi na siungi mkono kukwepa kodi ila kodi ziwe rafiki (ziwe zinalipika) kuna watu wamefunga biashara kwa madeni ya kodi kubwa makubwa kuliko faida
 
Wenye akili wameelewa ila kilaza kama wewe hauwezi elewa alichoamanisha
Inawezekana wewe ukawa unaupenda UKILAZA...

Mswahili hataki kulipa Kodi.....
Mswahil hataki /haweki kumbukumbu ya RISITI za mnyororo wa biashara.....

Mswahili anataka "shortcut" ya kila kitu.....awe ofisini/majeshini/uraiani.....

KODI ni wajibu kwetu......
 
Back
Top Bottom