Wafanyakazi wa TRA nanyi fungueni maduka Kariakoo mlipe kodi hizi

Wafanyakazi wa TRA nanyi fungueni maduka Kariakoo mlipe kodi hizi

Ndio maana Kuna mwaka nilienda Mbeya nikaenda pale Muanjerwa kununua nguo nikakuta bei rahisi sana kulinganisha na kariakoo nilipo muuliza mweji wangu akaniambia hizi nguo zinatoka Zambia

Ni kweli hi nchi Ina vilaza wengi maana hapo wanaofaidika kupitia bandari yetu sio tu wafanya biashara wa Zambia hata Serikali Yao pia inafaidika sana maana hao wafanya biashara wa Tanzania wanaponunua mizigo wanalipa na Kodi Kwa serikali ya Zambia

Na hao wazambia wanaomba tuendelee kulala na kuwa vilaza Ili waendelee kufaidika na ukilaza wetu
Upo sahihi zambia wanatoza kodi kidogo endelevu iyo inapelekea wafanyabiashara wapende kununua mizigo zambia tena na tena na Tanzania tuna toza kodi nyingi/kubwa kwa mara moja hivyo wafanyabiashara wengi wanakimbia na kusababisha mianya ya megendo
 
Japo wafanyabiashara wanachangamoto nyingi dhidi ya TRA lakini pia wapo wafanyabiashara wengi walaghai. Naona sana kwenye biashara zao hawatoi risiti na hata kama akitoa risiti basi kaiandikia pesa ya chini sana. Hv mtu ananunua mzigo wa milioni anaandikiwa risiti ya laki moja
Hata hiyo ndogo kajitahid sana mkuu.
 
Back
Top Bottom