Mazungumzo kwenye ukadiriaji kodi ndo mtiti. Mimi nimeingiza bidhaa, let's say, suti za kiume toka Uturuki za materio fulani. Nakadiriawa kodi milioni 200. Mtu mwingine kaagiza the same quality na quantity ya mzigo kama wangu. Kakadiliwa kodi milion 80 au pungufu ya hapo. Sasa unategemea hawa watu wawili kwenye soko itakuwaje?
So far, kodi ni nyingi na nyingine hazina majina na zina highest rates ambazo hazilipiki, na sheria hazitekelezeki.
Kuna biashara za wakubwa hazitozwi kodi na biashara za wengine wasio kuwa na nasaba au muhali na viongozi zitozwe utitiri wa kodi. Hapo ni ngumu wengine kulipa kodi na kufanya biashara.
Ushauri wangu:
- Rates za kodi zipunguzwe, na ikiwezekana hata VAT iwe 10-12%.
- Sheria za kodi ziangaliwe upya na zirekebishwe kwa maslahi ya taifa.
- Teknolojia rafiki itumike kwenye ukusanyaji wa kodi.
- Liundwe jeshi kamili kudhibiti magendo na watumishi wa TRA, TPA, na mamlaka za udhibiti ambazo zinahusika pale ambapo mtumishi ata miconduct, kama kusababisha urasimu, rushwa, nk.
- Elimu itolewe kila mwananchi atambue umuhimu wa kulipa kodi, sambamba na kila mwananchi ahiari na ashurutishwe kulipa kodi.
Ni wangu mtizamo. Naruhusu kupingwa kwa hoja.