Wafanyakazi wa TRA nanyi fungueni maduka Kariakoo mlipe kodi hizi

Mojawapo ya madai yao ni risiti za kueletroniki na uhalisia wa biashara na faida na matumizi
 
Mojawapo ya madai yao ni risiti za kueletroniki na uhalisia wa biashara na faida na matumizi
Lipa kodi acha longolongo....

Jifunzeni kwa WAHINDI shubamit.....
Ukiacha uchawi wako utaelewa
 
Mazungumzo kwenye ukadiriaji kodi ndo mtiti. Mimi nimeingiza bidhaa, let's say, suti za kiume toka Uturuki za materio fulani. Nakadiriawa kodi milioni 200. Mtu mwingine kaagiza the same quality na quantity ya mzigo kama wangu. Kakadiliwa kodi milion 80 au pungufu ya hapo. Sasa unategemea hawa watu wawili kwenye soko itakuwaje?

So far, kodi ni nyingi na nyingine hazina majina na zina highest rates ambazo hazilipiki, na sheria hazitekelezeki.

Kuna biashara za wakubwa hazitozwi kodi na biashara za wengine wasio kuwa na nasaba au muhali na viongozi zitozwe utitiri wa kodi. Hapo ni ngumu wengine kulipa kodi na kufanya biashara.

Ushauri wangu:

  1. Rates za kodi zipunguzwe, na ikiwezekana hata VAT iwe 10-12%.
  2. Sheria za kodi ziangaliwe upya na zirekebishwe kwa maslahi ya taifa.
  3. Teknolojia rafiki itumike kwenye ukusanyaji wa kodi.
  4. Liundwe jeshi kamili kudhibiti magendo na watumishi wa TRA, TPA, na mamlaka za udhibiti ambazo zinahusika pale ambapo mtumishi ata miconduct, kama kusababisha urasimu, rushwa, nk.
  5. Elimu itolewe kila mwananchi atambue umuhimu wa kulipa kodi, sambamba na kila mwananchi ahiari na ashurutishwe kulipa kodi.
Ni wangu mtizamo. Naruhusu kupingwa kwa hoja.
 

[emoji2956]

Comment ya kizalendo....
Comment bora kabisa.....[emoji120]
 
Mojawapo ya madai yao ni risiti za kueletroniki na uhalisia wa biashara na faida na matumizi
 
Mojawapo ya madai yao ni risiti za kueletroniki na uhalisia wa biashara na faida na matumizi

Ukiacha uchawi wako utaelewa
Bora ya mchawi kuliko MKWEPA KODI......lipa kodi uendelee kuwa MSAFI WA MATENDO....karibu kilingeni[emoji120]
 
Kwahiyo hao wafanya biashara waliofunga maduka kariakoo Kwa kero za TRA wote ni vilaza ila wewe ndio mwenye akili

Believe me wewe ndio kilaza
 
Hivi kwa zama hizi za mifumo ya kieletronic tra inashindwa Nini kuweka mifumo ya kutrack imports na sales za wafanyabiashara bada ya kucheza sandakalawe?
Maana kwa utaratibu huu wenye uwezo WA kukwepa ndio wanalipa kidogo wakati wale wasio na means za kukwepa wanakamuliwa kuzipa pengo
 
Kwahiyo hao wafanya biashara waliofunga maduka kariakoo Kwa kero za TRA wote ni vilaza ila wewe ndio mwenye akili

Believe me wewe ndio kilaza
Neno kilaza sikulianza mimi bali wewe ukimwambia the boss na ndio maana nikaandika "unapenda ukilaza/vilaza"....ok mgosi sasa unautafuta msamiati ulio sahihi......

Mgosi ni hivi....hata muuaji wa kweli anajitetea mahakamani kupitia yeye binafsi na wakili wake.....

Hao wafanyabiashara wanatetea maslahi yao.....wana haki hiyo.....kwani duniani kote mfanyabiashara anataka maximization of profit tu....hizo nchi zilizoendelea wameweka utaratibu wa lazima wa kulipa kodi....kupitia elimu ya kodi kwa kila mwananchi.....wananchi na wafanyabiashara wao wanaelewa.....ngoma iko kwetu sisi Waswahili......hatutaki/hatupendi kuweka risiti ya mlolongo wa biashara zetu....kwetu ni "shortcut" tu....sasa huo uhuru tutakao unapatikana wapi ??!!!

Kulipa kodi ni sawa na zaka za dini.....zaka si sadaka na si hiyari......

Lipa kodi acha "umbubu"......
 
Kodi isiyolipika wanashangilia wachawi pekee
[emoji1787][emoji1787]
Unazungukazunguka kwa kutaka "shortcut".... lipa kodi tuwalipe walimu wanaotufundishia watoto wetu, tuwalipe askari wanaotulinda, tujenge barabara na zahanati......

Ukija KILINGENI kwangu hakuna MAVUMBA na HIRIZI za kukwepa kulipa kodi [emoji1787][emoji1787]
 
Nyie wafanyabiashara wa kariakoo ndio hamjielewi asa hapo t.r.a wamekosa nn? wao wanafanya kazi Kwa mujibu wa Sheria zilizopitishwa na wabunge wenu na kusainiwa na rais wenu uyo mnaemuona kama kimbilio.

Wakati haya mamb ya Kodi yanajadiliwa bungeni mnajifanya mpo bize na biashara,kuja kushtuka yashapitishwa mnakumbana na matokeo mnaanza kulialia na migomo isiyoelezeka..


T.r.a wanatelekeza wajibu waliopewa na muajiri wao ambae ni uyo serikali ya mama Samia na kasimu wake...
 
Maduka wanayo mkuu pale kariakoo ila ni FREE OF CHARGE.Sikuzote wanaoteseka ni maskini na wote wasio na watetezi
 
Hujielewi
WEWE ndio hujielewi sabb hao TRA wanatimiza wajibu wao waliopewa na mwajiri wao uyo Samia na kasimu majaliwa... Sasa wewe unashupaza shingo kuwaattack TRA as if ndio waliopitisha hzi Kodi na kuzisaini wao...

Wakati hizi Kodi zinajadiliwa bungeni na wabunge wenu mlikua mpo bize na biashara zenu sasa yamewakuta... mnaanza lialia
 
Ulipojifunza kuhusu hyo biashara ya suti nazani ulijifunza mengi ndipo ukaamua kuingia umo..kosa Moja watz wanafanya ni kutojifunza kuhusu Mamb ya Kodi na Sheria zake ktk biashara husika anayotaka kufanya..

Kama ulitumia mda na gharama kujifunza kuhusu bidhaa Yako,tabia za wateja, pricing,how to transport nk why not hukujifunza kuhusu mamb ya Kodi na Sheria za nchi ktk hyo biashara Yako? Kodi na biashara ni mapacha Kila sehem hivo ni busara sana kujua mamb ya Kodi ktk biashara Yako ili ujue unatokea wap na unaingilia wapi, ukionewa na TRA ujue Kwa facts!!! sio bla bla tu..

binafsi nafanya biashara ya kukopesha microcredit. Awali nilisumbuka sana na hao watu. Nikachukua mda na gharama kiasi nikatafuta wabobez WA mamb ya Sheria na Kodi ktk tasnia yangu. Sasa naenda sawa na hao TRA coz wanajua najua!!!

Wewe mfanyabiashara jifunze mb ya Kodi ktk biashara Yako na Sheria za nchi kuhusu biashara Yako.
 
Wafanya biashara sio kama hawataki kulipa Kodi ishu iliyopo ni hizo sera TRA kuusu hayo malipo ya Kodi

Mfano halisi kama sera zetu zimetungwa na vilaza ni hu

Kontena la vitenge kutoka China bandari ya Kenya linatoka Kwa ushuru wa 45M

Kontena kama hilo katika bandari ya Daresalaam linatoka Kwa ushuru wa 300M

Matokeo ya ubovu wa sera za Kodi za TRA zinatufanya Watanzania tuende tukachukue mzigo Zambia au Malawi ndio unakuwa na nafuu kuliko ukiagiza kutoka China

Kibaya zaidi hiyo mizigo ya Zambia na Malawi yote imepitia katika bandari yetu ya Daresalaam

Yani badala Tanzania ilishe wafanya biashara wa nchi zisizo na bandari imekuwa kinyume chake wafanya biashara wa Tanzania walishwa bizaa na nchi ambazo hazina bandari

Kwa lugha rahisi wafanya biashara wa nchi zisizo na bandari wanafaidika na bandari yetu kuliko wafanya biashara wetu

Hi nchi Ina vilaza wengi sana
 
Bora ya mchawi kuliko MKWEPA KODI......lipa kodi uendelee kuwa MSAFI WA MATENDO....karibu kilingeni[emoji120]
TRA kila mwaka ukienda kukadiliwa kodi inapanda hawajui kama mwaka huo ulipata hasara au laa, mfanyakaz uwez ukarijua hili sababu wewe sio risk taker, na kitanda usicho kilalia kamwe uwez jua kunguni wake
 
Tra anahusikaje na Bima ya afya?
Umeme?
Ulinzi?
Mishahara ya wafanyakazi wako?

Ada za watoto wako??


Hivi vyote ndo visingizio msilipe kodi???


Lipeni Kodi ....
Tangu jana unajitoa sana ufahamu

Tushakujua
 
Ndio maana Kuna mwaka nilienda Mbeya nikaenda pale Muanjerwa kununua nguo nikakuta bei rahisi sana kulinganisha na kariakoo nilipo muuliza mweji wangu akaniambia hizi nguo zinatoka Zambia

Ni kweli hi nchi Ina vilaza wengi maana hapo wanaofaidika kupitia bandari yetu sio tu wafanya biashara wa Zambia hata Serikali Yao pia inafaidika sana maana hao wafanya biashara wa Tanzania wanaponunua mizigo wanalipa na Kodi Kwa serikali ya Zambia

Na hao wazambia wanaomba tuendelee kulala na kuwa vilaza Ili waendelee kufaidika na ukilaza wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…