MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 21,387
- 44,030
Mkuu hakuna redio ya mjini wala kijijini ambayo haijaathiriwa na social media. Tena huko mikoani ndo hali tete zaidi. Hizo project unazosema huwa ni mara chache na kwa redio chache zitakazobahatika. Mbaya zaidi ni kuwa hadi upate huo mchongo kuna watu lazima nao wapate mgawo wao. Redio za mikoani ndo hulipa watangazaji laki 1 hadi laki na nusu. Kwa mfano Radio 5 Arusha huwa wanaweza fika hata miezi 8 hawajalipa mishahara.Hata kama ungekuwa wewe mkuu
Unataka kufanya projects ya afya wilaya za mkoa wa Tabora. Huwezi kupeleka matangazo yako Clouds au EFM.
Sasa hivi NGO labda na wizara ya afya wanapeleka matangazo kwenye local radio za wilaya kwasababu ndio ziko kwenye eneo la projects.
Radio za wilayani huko ndani ndani Nenda kazisikilize utakuta matangazo wanayo mengi sana.
Kuna radio Moja pale Mbeya imejaa matangazo ya solar na miradi ya afya katika wilaya hiyo.
Matangazo wanayopeleka EFM au Clouds ni yake ya NATIONAL LEVEL
Nadhani unapata picha
Hao Kwizera walilamba Dili la NGO PLAN international kwenye education awareness. Ni Hela nyingi. Na huwezi kusikia hizo local/ district radio eti zinayumba.
Advantage Yao ni kuwa wako kwenye population ya wanufaika wa miradi mingi ya serikali na NGO.
Kwa mfano wanunuaji wa solar wako huko wilayani sio Dar Sasa kampuni ya solar itapelekaje matangazo EFM Ambayo hata vijijini haisikiki wakati huko wilayani kwenye hizo project Kuna radio zinasikika Hadi vijijini