JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Wakili wa Serikali, Monica Mwela amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Dastan John Charles (23), Christopher John Charles (23), Emmanuel Joshua Olala(24) ambao ni wakazi wa Kilangalanga Mlandizi pamoja na Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Emmaeli Lukumai amesema ushahidi wa kesi hiyo iliyosomwa kwa mara ya kwanza bado haujakamilika, hivyo kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 30 mkwaka huu.
Wakati wakisomewa kesi hiyo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.
Chanzo: AZAM TV
Pia soma ~ Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo