Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia

Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia

Yawezekana mdaiwa alitumia nguvu nyingi sana ikapelekea na wao kutumia nguvu zaidi Ili kumdhibiti vinginevyo pengine angewauwa wao ni bora afe mmoja kuliko wangekufa watu wanne
Una habari kuwa mdaiwa alikuwa nyumbani kwake na wao ndiyo walimvamia? Kuna sheria inasema uingie kwenye nyumba ya mdaiwa na kuiba vyombo vyake. Huu ni utetezi wa kijinga sana hauna ground yoyote.
 
Aiseeee kampuni inaajiri vitoto vidogo na kuwatwika majukumu makubwa.
Bosi wao naye aswekwe ndani
Wanaambiwa mshahara laki 240,000/= ikifika mwisho WA mwezi wanapigiwa mahesabu na kulipwa Kwa kuangalia wamedai kiasi gani. KIJANA wangu alipata kazi huko nikamkatalia. Alinishukuru Kwani wenzie waliompeleka wadhulumiwa. Vijana wasipodai hawalipwi ndio maana wanatumia Hadi NGUVU 😔
 
Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia ya Juma Said Seif (45), mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi Mkoani Pwani yaliyofanyika Oktoba 7. 2024.

Wakili wa Serikali, Monica Mwela amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Dastan John Charles (23), Christopher John Charles (23), Emmanuel Joshua Olala(24) ambao ni wakazi wa Kilangalanga Mlandizi pamoja na Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Emmaeli Lukumai amesema ushahidi wa kesi hiyo iliyosomwa kwa mara ya kwanza bado haujakamilika, hivyo kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 30 mkwaka huu.

Wakati wakisomewa kesi hiyo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.

Chanzo: AZAM TV

Pia soma ~ Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Wana roho mbaya sana hawa vijana
 
Huyu mwenye Bichwa Refu Anyongwe haraka
 
Vijana wengine wa hovyo ni wale ambao wametoka jkt aisee ni wangese wanajifanya wababe kinoma kisa walikuwa wanajifunza mbio huko kambini
 
Wanaambiwa mshahara laki 240,000/= ikifika mwisho WA mwezi wanapigiwa mahesabu na kulipwa Kwa kuangalia wamedai kiasi gani. KIJANA wangu alipata kazi huko nikamkatalia. Alinishukuru Kwani wenzie waliompeleka wadhulumiwa. Vijana wasipodai hawalipwi ndio maana wanatumia Hadi NGUVU 😔
Aiseee hii kesi mwajiri kujitoa si sawa.
Ashikwe na yeye
 
BoT inapaswa ichunguze mikopo inayo tolewa na taasisi za mikopo.
Inashangaza mikopo umiza bado inakuwa kero kwa wananchi hadi inaletelezea mauaji.
Pia Mabanki mengi bado yanawanyonya wananchi kwenye mikopo. BoT wamelala kama vile hawaoni!!!!
 
Hata kama vipi huwezi kunfata unaemdai saa 10 usiku ! Hii haikubaliki ! Kwa nini wasimfuate mchana ?? Kama wameshindwa basi kuna taratibu za keshiria zimewekwa na nchi ! Lakini waliamua kuwa polisi wao mahakama wao ! Hii nchi hiiiii ! Bado wale washenz wa mitandaoni wakiwatishia watu eti utaona ! Leo tuone kama utafika mpaka jioni ! Na vitisho viingi vya ajabu ajabu.Hawa OYA , viongozi wao pia inabidi washtakiwe kwa kosa la mauaji na mahakama ndo itaamua kama wanahusika au la ! Kwa sababu wao ndo walibariki hao wapuuzi kwenda kuuua.Waondolewe veli walizovaaa wapelekwe mahakamani wakajitetee
 
Back
Top Bottom