Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia

Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia

Hizi microfinances zimekuwa na vituko na mambo ya ajabu.
Mi ndio maana kwenye biashara hizi naweza kusikiliza mawazo ya mtu kuhusu biashara anayotaka kufanya nikamsikiliza akaongeaa nikampa moyo lakini kichwani najua huyu hatoki.

Na imetokea mara nyingi, inakuwa hivyo.

Sasa hawa matajiri wanao invest kwenye hizi microfinance uchwara, sijui apps, unatoa millions kutengeneza apps hali ya kuwa tabia ya asili ya mtanzania inajulikana ni wagumu ile mbaya kulipa madeni.

Kuna biashara baadhi ya nchi huwezi fanya tokana na asili ya watu.

Matokeo yake ndio haya, mara kutumiana sms za kutishana, haya wamepigana wameua...

Biashara zingine tumia akili tu, tena akamatwe na tajiri.
 
Akili ni kwa ajili ya kufikiri tu,kwahiyo ndio maana tunaoa kwasababu sisi sio wanyama,tunajua hatuwezi kuparamiana siku zote au katika maisha yetu yote

busara ni kuliweka kila jambo mahala pake hiyo ndio maana ndogo ya busara

sasa ni wachache sana wanaliweza hilo lkn at 40's unakuwa na nyenzo hiyo
Unapoeleza kwamba akili ni kwa ajili ya kufikiri tu unamaanisha nini?Kwamba mtu anakuwa na ukomo wa kuitumia akili?Kwamba mtu anakuwa na uchaguzi wa baadhi ya mambo ili atumie akili?
SWALI:Hao vijana akili zao zilijilazimisha kutumika kutafuta vurugu,ugomvi hadi kuua tu bila hizo akili zao kuchagua amani,suluhu na kuomba usaidizi wa viongozi au kisheria?
 
Walikuwa na akili ya kukusanya deni tu na ndio maana walifanya waliyofanya,yani akili iliwapa option moja tu walipwe hela yao ndio walivyofikiri

Maana ishu ilikuwa mke kakopa bila mume kujua,kwahiyo ilitakiwa mke awepo athibitishe hilo

Busara ingewataka waliweke kila jambo mahala pake,na mahala pake ni kumsubiri mke awepo athibitishe hilo deni mbele ya mumewe na kuchukua dhamana period
 
Basi kampuni imeajiri vichaa ambao hawajui wala hawawezi kutumia hizo akili zao kulingana na mazingira husika.
 
Umri si hoja.Mob psychology,kupokea maagizo ya mwajiri bila kuyachuja kama ng'ombe,kutanguliza undava,kutokukubali kushindwa na mazoea ya waliyokuwa wanawafanyia wengine iliwafanya kutotumia akili kuepusha dhahma.
Sio kwamba hawakutumia akili,walitumia ndio maana walienda katika nyumba ile na si kwako Moisemusajiografii ,hawajatumia bussara
 
Naamini wapo kwenye majuto makuu. Honestly nawaonea huruma kama vijana wenzangu ila ndio hivyo kuna mtu kapoteza mzazi.
 
Ningekuwa hakimu ningewapata na kosa la involuntary manslaughter sio murder na kisha kuwapunguzia adhabu kwa sababu hawakukusudia na walimkimbiza hospital.
Sema maisha haya, hapo hakuna hata mmoja ambaye aliwahi fikiria ipo siku atashtakiwa kwa kuua aisee.
Life ni upofu mkuu
 
Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia ya Juma Said Seif (45), mkaazi wa Kitongoji cha Mbagala Mlandizi Mkoani Pwani yaliyofanyika Oktoba 7. 2024.

Wakili wa Serikali, Monica Mwela amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Dastan John Charles (23), Christopher John Charles (23), Emmanuel Joshua Olala(24) ambao ni wakazi wa Kilangalanga Mlandizi pamoja na Abdallah Felix Wendiliwe (32) mkaazi wa Janga Mlandizi.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kibaha, Emmaeli Lukumai amesema ushahidi wa kesi hiyo iliyosomwa kwa mara ya kwanza bado haujakamilika, hivyo kesi hiyo imehairishwa hadi Oktoba 30 mkwaka huu.

Wakati wakisomewa kesi hiyo, watuhumiwa hawakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji. Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.

Chanzo: AZAM TV

Pia soma ~ Kampuni ya OYA watoa milioni 1 kwa familia Juma Mfaume ambaye alifariki baada ya kupigwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo
Aisee..
Maisha yanaweza badilika muda wowotee...

Sad!
 
Back
Top Bottom