Wafanyakazi wanne wa taasisi ya mikopo ya OYA wafikishwa Mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya kukusudia

Yawezekana mdaiwa alitumia nguvu nyingi sana ikapelekea na wao kutumia nguvu zaidi Ili kumdhibiti vinginevyo pengine angewauwa wao ni bora afe mmoja kuliko wangekufa watu wanne
Hawakutakiwa kutumia nguvu hata kidogo ni kinyume na sheria kwa taasisi ya fedha hii imekula kwao
 
Kumpeleka hospitali inaonesha hawakukusudia kuua. Wakipata mwanasheria mzuri anaweza kuwasaidia kubadili kesi, ila kifungo hakiepukiki.
 
Naona wote under 40, umri wa mihemuko kuliko busara. Mungu awavushe salama.
 
Kama ni hivyo,wote tungekufa au kupata dhahma mbaya kwenye umri mdogo.Ili twende sawa,tutumie neno AKILI isikuletee ukakasi kwenye tafsiri.
Siko hapa kukwepa ukakasi nipo hapa kusema ukweli,binadamu akifika miaka arobaini ndio anakuwa amekomaa,ndio maana wanasema maisha yanaanza kwenye miaka 40

Hata mitume wengi walipewa utume walipofikia miaka 40

Hata katiba ya tanzania raisi afikie miaka 40

Chini ya hapo ni kuokoteza tu
 
Ingekuwa hivyo hata kuoa/kuolewa ingekuwa ni hadi watu wafike miaka 40.Kuna mambo hayahitaji ubishi au kuonesha ukakamavu.Akili itangulie kwanza.Think before you do anything.
 
Na
Naendesha na kumiliki kampuni ya ukusanyaji wa madeni, huwa nahamasisha Sana collection instead of recovery haswa yenye utumiaji wa nguvu na pia inanisaidi kuondoa a na kesi za madai za kila leo, kwangu na kwa wateja wangu na bado inaacha mazingira ya urafiki na sio uadui
 
Walianza kuongea.Wakaja kufokeana.Wakaenda mbele kutukanana na kutishiana.Hawakuishia hapo,wakatafuta gongo.Wakampiga(sijajua ni mara ngapi).Baada ya kuona wamejeruhi na wametambulika ni wafanyakazi wa OYA na hawana ujanja tena wa kuhepa dhahma ndiyo wakamkimbiza hospitali.Sidhani kama huruma ndiyo iliwaongoza.Na,haijulikani kama mdaiwa alifia palepale,njiani au hospitali!
 
Ingekuwa hivyo hata kuoa/kuolewa ingekuwa ni hadi watu wafike miaka 40.Kuna mambo hayahitaji ubishi au kuonesha ukakamavu.Akili itangulie kwanza.Think before you do anything.
Akili ni kwa ajili ya kufikiri tu,kwahiyo ndio maana tunaoa kwasababu sisi sio wanyama,tunajua hatuwezi kuparamiana siku zote au katika maisha yetu yote

busara ni kuliweka kila jambo mahala pake hiyo ndio maana ndogo ya busara

sasa ni wachache sana wanaliweza hilo lkn at 40's unakuwa na nyenzo hiyo
 
Akili za kuambiwa changanya na zako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…