Wafikishwa Mahakamani kwa kudukua Mfumo wa Kompyuta wa CRDB

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB na kujipatia kiasi cha Sh Milioni 13.8.

Washtakiwa hao ni Riziki Kanena (22) ambaye ni mkazi wa Mikocheni na Laulentina Yastaf Mkazi wa Akamea Karagwe mkoani Kagera.

Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.

Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.

Pia katika shtaka la nne linalomkabili Laulentina , inadaiwa tarehe hiyo akiwa eneo la Akamea Karagwe mtaa wa Mlamba vijijini mkoani Kagera alipokea Sh. Milioni 5.4 wakati akijua ni mali ya wizi.

Aron amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema washtakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Pamela, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14,2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

BONGO 5
Miaka 22 ameshaanza kuiba? Atafika kweli huyo, inasikitisha badala atumie hiyo akili kuzalisha uchumi upae yeye anatumia akili kuiba kazi iliyolaaniwa na mwenyenzi Mungu.
 
Tulia wewe punguza kelele wameambiwa wasijibu chochote maana Mahakama hio haina jurisdiction utaona wanavyoipangua hio kesi hakuna kesi hapo
 
Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB na kujipatia kiasi cha Sh Milioni 13.8.

Washtakiwa hao ni Riziki Kanena (22) ambaye ni mkazi wa Mikocheni na Laulentina Yastaf Mkazi wa Akamea Karagwe mkoani Kagera.

Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.

Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.

Pia katika shtaka la nne linalomkabili Laulentina , inadaiwa tarehe hiyo akiwa eneo la Akamea Karagwe mtaa wa Mlamba vijijini mkoani Kagera alipokea Sh. Milioni 5.4 wakati akijua ni mali ya wizi.

Aron amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema washtakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Pamela, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14,2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

BONGO 5
Dah!...huyu kijana mdogo amesomea 'IT' au 'programming' nini ?...ana akili nzuri sana, sema ameitumia vibaya.
 
Haya wahaya kaeni mkao wa kiadivoketi kuikwamua ndege ziwani.
 
Hapo imepambwa kama ni udukuzi ila kiuhalisia hakuna udukuzi uliofanyika
Huu sio udukuzi.
👇
Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.
 
Wanatakiwa wapewe pongezi maana kama mtu wa ndani mtanzania ameona udhaifu kwenye mfumo wao ina maana amewaokoa wasiibiwe fedha nyingi zaid na mtu wa nje si kila kosa la kumuukumu mtu mengine ni funzo watu wajifunze na vitengo wa one umuhimu wa hao vijana
Kuna mtu wa ndani amewapa details. Narudia tena. Kuna mtu ndani amewapa details!
 
Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.
Haya maelezo ni tofauti na tafsiri yako ya udukuzi stow away
 
Back
Top Bottom