Wafikishwa Mahakamani kwa kudukua Mfumo wa Kompyuta wa CRDB

Wafikishwa Mahakamani kwa kudukua Mfumo wa Kompyuta wa CRDB

Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB na kujipatia kiasi cha Sh Milioni 13.8.

Washtakiwa hao ni Riziki Kanena (22) ambaye ni mkazi wa Mikocheni na Laulentina Yastaf Mkazi wa Akamea Karagwe mkoani Kagera.

Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.

Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.

Pia katika shtaka la nne linalomkabili Laulentina , inadaiwa tarehe hiyo akiwa eneo la Akamea Karagwe mtaa wa Mlamba vijijini mkoani Kagera alipokea Sh. Milioni 5.4 wakati akijua ni mali ya wizi.

Aron amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema washtakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Pamela, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14,2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

BONGO 5
Ila vigogo wao wa serikali wanavyotuhujumu kila kukicha wakipelekwa mahakamni wanapewa nafac ya kujitetea, Thats why i hate the existence of Government its always hypocritical
 
Huu sio udukuzi.
👇
"" Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.""

Umesoma hapo???
 
Nashauri kwa yeyote alie na Nia ya kuiba Bank pasipo kutumia siraha akajifunze kupitia Mikasa miwili adhimu na iliyoitikisa Dunia.
1) Ni ule mkasa wa SPAGIARI na GENGE lake

2) Na mkasa wa pili ni ule mkasa wa wale wadukuzi wawili waliodukua mifumo ya bank na kuiba kiasi cha zaidi ya billion 200 za kitanzania bila kujulikana hadi leo, huu mkasa ulisukwa kwa ustadi mkubwa Sana. kuanzia liletukio la wale jamaa kwenda kufungua account 4 bank na ku deposit pesa kiasi cha Dola miatano kwenye kila account na kuzitelekeza kwa zaidi ya miezi minne,, aiseeee
haya mambo yanapaswa kifundishwa level fulani ya elimu hapa kwetu na sio kuwakalilisha watu Integration na madudu mengine mengi,

Dunia inabadilika
 
Hv we uliyeleta hii habar unajua uzito wa hi sentensi “kudukua mfumo wa bank”!???
 
Watu wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka manne likiwemo la kuingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB na kujipatia kiasi cha Sh Milioni 13.8.

Washtakiwa hao ni Riziki Kanena (22) ambaye ni mkazi wa Mikocheni na Laulentina Yastaf Mkazi wa Akamea Karagwe mkoani Kagera.

Wakili wa Serikali,Titus Aron akiwasomea mashtaka hayo amedai kati ya Januari 3, 2023 na Juni 3, 2023 mshtakiwa Riziki akiwa Mikocheni wilaya ya Kinondoni kwa nia ovu aliingilia mfumo wa kompyuta wa benki ya CRDB kisha kujipatia kiasi cha Sh.Milioni 13.8.

Imedaiwa kuwa tarehe hizo mshtakiwa Riziki alitumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la Yusuph Mboko kisha aliiba kiasi hicho kwa kutumia laini ya simu ya Mboko bila kutoa taarifa kwa umiliki wa mtandao.

Pia katika shtaka la nne linalomkabili Laulentina , inadaiwa tarehe hiyo akiwa eneo la Akamea Karagwe mtaa wa Mlamba vijijini mkoani Kagera alipokea Sh. Milioni 5.4 wakati akijua ni mali ya wizi.

Aron amedai upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo aliomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo amesema washtakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi.

Hakimu Pamela, ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 14,2023 kwa ajili ya kutajwa na washtakiwa hao wamerudishwa rumande.

BONGO 5

Nashauri waajiriwe huko benk kama ma IT
 
Uki
Wanatakiwa wapewe pongezi maana kama mtu wa ndani mtanzania ameona udhaifu kwenye mfumo wao ina maana amewaokoa wasiibiwe fedha nyingi zaid na mtu wa nje si kila kosa la kumuukumu mtu mengine ni funzo watu wajifunze na vitengo wa one umuhimu wa hao vijana
Ukiona mapungufu sio unaiba mzee,toa taarifa rasmi itakua rahisi kupewa michongo kwny taasisi husika
 
Uki

Ukiona mapungufu sio unaiba mzee,toa taarifa rasmi itakua rahisi kupewa michongo kwny taasisi husika
Wengi wamefanya hivo wameambulia Asante na ki laki bas ata ajira hawapewi shida hamna anaye tambua mchango wao watu wamesoma sana na wanaujuzi sana ila kutambulika na serikali au jamii ni ngumu kilicho Baki ni kuwaonesha Kwa vitendo na miaka ijayo kama tutaendelea kuzalisha wasomi tu bila kuwa n mikakati basi tutakuwa kama Nigeria wasomi wengi ila wezi ndio ajira pekee
 
Dah!...huyu kijana mdogo amesomea 'IT' au 'programming' nini ?...ana akili nzuri sana, sema ameitumia vibaya.
Kuiba simu ya mtu unayejua password yKe ya simbanking ni kusoma IT
 
Hao hawadukua mifumo ya kompyuta bana.
 
Back
Top Bottom