Wafuatao wamefunga ndoa na umaskini. Na ni ngumu ndoa zao kuvunjika

Wafuatao wamefunga ndoa na umaskini. Na ni ngumu ndoa zao kuvunjika

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
14,588
Reaction score
32,361
Umaskini ni fedheha. Kwenye maisha yako yote chukia umaskini kwa kila hali. Fanya jambo lolote la halali kujiondolea umaskini kwenye maisha yako. Ibara ya 25 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetamka wazi namna ya kuondokana na umaskini. Hata Mwenyezi Mungu mwenyewe hataki viumbe wake tuwe maskini.

Mengi sana yamesemwa kuhusu umaskini ila mimi leo ninayataja makundi ambayo ni ngumu sana kwao kujichomoa kwenye umaskini. Ni kama wamefunga ndoa na umaskini. Kama unaangukia kwenye kundi mojawapo basi badilika kabla hujachelewa.

1. Kundi namba moja ni wale wanaopambana sana kujitafuta na kweli kuna wakati riziki zinawajia ila cha kusikitisha wakipata hela kidogo kama sio kuongeza mke basi ataongeza mpenzi au mchepuko.

2. Wale wanaotumia vibaya msemo wa "Tutafute hela ila tusisahau kuishi" ni kundi namba 2 lililofunga ndoa na umaskini. Hili kundi wengi wao ni kipato cha kati. Badala ya kuwekeza vizuri vipato vyao hutumia kufurahisha nafsi zao kwa kisingizio cha "tusisahau kuishi".. mara nyingi huchukua mikopo ya magari na vacations. Wengi wao kukitokea hitilafu kidogo kwenye kazi zao huwa ni kilio. Tumia sehemu ya faida kula maisha na sio mtaji.

3. Wajasiriamali wadogo wanaoanza kuinuka ila katika hali ya kushangaza badala ya kukuza zaidi biashara yao husombwa na kelele za jamii kununua kiwanja na kuanza kujenga nyumba pamoja na kununua gari ya kutembelea. Hili ni kosa kubwa sana linalofanywa na vijana wengi wadogo wanaoanza kujitafuta. Hili kundi lina wanamichezo na wasanii pia. Kwa mfano mwanariadha ukishinda mbio ukalipwa labda Tsh 10m tafadhali achana na habari za kurudi kijijini na kuanza kusimamia ujenzi. Nenda hata kalipie kambi Eldoret au Ethiopia ufanye mazoezi na mabingwa.

4. Wanaochukua mikopo kugharamia harusi au sherehe nyingine yoyote ya gharama.

5. Wale watu wanaotumia fedha zao kufungulia biashara wasizozifahamu hata kidogo kisa wameambiwa inalipa. Mara nyingi wastaafu wako kwenye hili kundi.

6. Wote wasiojali afya zao. Afya ni asset. Bila afya mambo mengine ni ubatili. Fanya uwezalo kuchukua tahadhari kuhusu afya. Ingawa kuumwa na kufa ni lazima lakini ukichukua tahadhari hata kidogo inapunguza sana mateso ukiwa hai.

7. Wenye visingizio kwenye suala zima la mawasiliano. Mtu anachukulia poa kutomiliki hata simu ya kitochi kiasi kwamba kupatikana kwake huwa ngumu mno. Au mwingine ana simu ila visingizio kama vile simu ilikuwa kwenye chaji, spika mbovu, simu ilikuwa silent, sikuona message yako, na visingizio vingine kama hivyo. Mtu yeyote kwenye huu ulimwengu wa digital ambaye kwake mawasiliano sio kipaumbele basi kafa kaoza kwa babe wake umaskini.
 
Inaonekana bado mdogo kiumri na ujajua siri y maisha kwaiyo unaongea kulingana na unavyosikia ila tambua kuwa utajiri si kwa wote na umaskini si kwa wote na maisha hayana formula cha msingi ni kuomba mungu uwe katika kundi zuri kuna watu wamejituma sana na wanapambana sana ila bado kujipata na kuna wanachezea pesa kila kitu na wamejipata na wanaendelea jipata
 
Inaonekana bado mdogo kiumri na ujajua siri y maisha kwaiyo unaongea kulingana na unavyosikia ila tambua kuwa utajiri si kwa wote na umaskini si kwa wote na maisha hayana formula cha msingi ni kuomba mungu uwe katika kundi zuri kuna watu wamejituma sana na wanapambana sana ila bado kujipata na kuna wanachezea pesa kila kitu na wamejipata na wanaendelea jipata
Sijaandika kwa kubahatisha. Tatizo waafrika wengi kwenye nyuzi kama hizi mnakimbilia kujifariji kwa kumtaja Mungu na kuamini miujiza.
 
Acha umaku. Nipe hicho kinyeo chako nikuonyeshe kama ni mwanamke
Kulikoni Mkuu?

Unajiita mama Samia kumbe dume? Basi unahitaji mtarimbo mpumbavu wewe..

While we embrace the use of nicknames, it's reasonable to expect these pseudonyms to reflect one's gender. Opting for a name typically associated with the opposite gender, yet anticipating others to address you accurately, lacks practicality. Ni USHOGA.

Pathetic!
 
Back
Top Bottom