Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,506
Wafugaji wa kuku wa nyama na mayai wametakiwa kujisajili kisheria ili waweze kutambulika na kufanya kazi ya ufugaji kwa ufuata sheria zilizowekwa.
Imeelezwa kuwa wote ambao hawajasajiliwa lakini wanafanya kazi ya ufugaji kuku, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mpaka sasa takwimu zinaonyesha ni wafugaji 41 tu ndio wameshasajiliwa.
Mamlaka zinazohusika zimesema ni lazima kila mfugaji kuku kuwa na kitambulisho, na asiye nacho atachukuliwa hatua za kisheria.
Taarifa hio pia imedai kuwa hata wauzaji pia wa kuku na mayai ni lazima kuwa na vitambulisho hivyo.